Sunday, October 25, 2020

SUAREZ AMWANGUKIA MESSI ASAINI MKATABA MPYA BARCA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

 BARCELONA, Hispania

MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Luis Suarez, amemwangukia staa mwenzake wa timu hiyo, Lionel Messi, akimtaka kufuata nyayo zake kwa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Camp Nou.

Mabingwa hao wa Ligi ya La Liga walitangaza juzi kwamba, wameshakubaliana na nyota huyo wa timu ya Taifa ya Uruguay kumwongezea mkataba utakaomfanya awatumikie hadi mwaka 2021 na Suarez ana matumaini Messi ndiye atakayefuata kutokana na mkataba wake unamalizika 2018.

“Furaha yangu itakamilika endapo Messi vilevile ataongeza muda katika mkataba wake,” Suarez aliwaambia waandishi wa habari.

“Lakini kuongeza kwangu mkataba si ujumbe kwa Messi. Yeye ana umri wa kutosha wa kupambanua lipi ni zuri kwake,” aliongeza straika huyo.

Mapema wiki hii Messi alishindwa katika mbio za kuwania tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Ballon d’Or na hasimu wake  Cristiano Ronaldo, lakini  Suarez anasema kuwa mchezaji mwenzake huyo ndiye aliyestahili kutwaa taji hilo.

“Kila mmoja ana vigezo vyake binafsi,” alisema nyota huyo.

“Ila nasononeka sana, Leo ndiye aliyestahili kutwaa tuzo mwaka huu kutokana na vitu anavyolitendea soka na ni mzuri,” aliongeza.

Mkataba mpya wa Suarez utamfanya abaki  Camp Nou  hadi atakapofikisha umri wa miaka 34 na anaonekana kuwa wazi atamalizia soka lake Barca.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -