Friday, December 4, 2020

SUMU YA AL AHLY KUIUA MC ALGER

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA HUSSEIN OMAR

SUMU ambayo iliwatoa udenda Al Ahly mwaka jana, ndiyo ambayo Yanga wamepanga kuitumia kuiua MC Alger kwenye mchezo wao wa marudiano utakaofanyika kesho.

Kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, ameweka wazi kuwa watatumia mbinu muhimu za kiuchezaji uwanjani ili kupata matokeo mazuri yatakayowawezesha kusonga mbele, huku akisisitiza kwamba watakuwa makini sana katika dakika za lala salama.

Alisema walipocheza na Al Alhy, walimtumia mshambuliaji wao, Dinald Ngoma, muda wote na hivyo kuwazuia Al Ahly kupanda na kwa sasa Ngoma amerejea kikosini hivyo wamejipanga kutumia mfumo uleule dhidi ya MC Alger.

Kikosi hicho cha Yanga kimeondoka jana jioni na wachezaji 20 kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano utakaochezwa kwenye Uwanja wa Omari Hamadi mjini Algiers.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, uliwashuhudia Yanga wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na kiungo Thaban Kamusoko.

Mwambusi alisema ni faida kubwa kwao kuwa na Ngoma ambaye katika mtanange wa kwanza alicheza vizuri licha ya kutokea benchi katika dakika 55.

Mzimbabwe huyo ameshaifungia timu yake mabao nane tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kesho ataiongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo akiwa na ‘pacha’ wake, Amissi Tambwe, kwa sasa yuko fiti pia.

“Tuna Ngoma na Tambwe. Hakuna asiyewajua kazi yao uwanjani. Tuna kikosi kipana lakini kila mmoja ana umuhimu wake na kwa wakati wake. Tuna imani kuwepo kwao kikosini kutatusaidia kufanya makubwa huko (Algeria),” alisema Mwambusi.

Mwambusi aliongeza kuwa kitu kingine kinacholipa matumaini benchi la ufundi la timu hiyo ni rekodi nzuri waliyonayo pindi wanapocheza wakiwa ugenini.

“Tuna rekodi nzuri sana ugenini. Huwa tunacheza soka la kasi na jihadi. Kwahiyo, tuna imani kubwa ya kufanya vizuri ingawa tulipata ushindi mwembamba katika mchezo wetu wa kwanza,” alisema Mwambusi.

Kihistoria, katika miaka ya hivi karibuni, timu za Kaskazini mwa Afrika zimekuwa changamoto kubwa kwa Yanga.

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, timu za ukanda huo zimeitoa Yanga mara nne kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mwaka 2012, Yanga walitolewa na wababe wa soka la Misri, Zamalek, mwaka uliofuata ilikuwa ni zamu ya Al Ahly kuwatesa Wanajangwani hao.

Mwaka 2015, Etoile du Sahel wakaitoa mapema Yanga na miezi 12 baadaye Yanga wakaondoshwa na Al Ahly.

Katika hatua nyingine, wachezaji wa timu hiyo walijengwa kisaikolojia ikiwa ni pamoja na kuzoea hujuma ndogondogo za mashabiki wa nchi za Kiarabu kwa kuwa wamekuwa na ushangiliaji usio na staha unaoweza kuwaondoa wachezaji mchezoni.

“Mashabiki wao ni watu wenye vurugu lakini pia staili yao ya kushangilia ni kurusha fataki juu, tena zenye miale ya moto. Hilo lisiwasumbue hata kidogo,” alisema Mwambusi.

Lakini pia, Mwambusi aliwataka wachezaji hao kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu ili kuepuka kadi zisizo na ulazima.

“Waarabu ni wajanja kwa kutengeneza kadi nyekundu kwa timu pinzani. Nidhamu ya mchezo ndio itakayotufanya kumaliza mchezo tukiwa wachezaji 11 uwanjani,” alisisitiza kocha huyo wa zamani wa Mbeya City.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -