Tuesday, October 20, 2020

SUNDAY MANARA ALIBATIZWA JINA LA ‘COMPUTER’ AKILINGANISHWA NA MASHINE INAYOFANYA HESABU HARAKA SANA

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA HENRY PAUL

UNAPOZUNGUMZIA wachezaji wa Tanzania waliocheza soka kwa kiwango cha juu, kamwe huwezi kuacha kulitaja jina la kiungo mshambuliaji Sunday Manara au Computer kama wapenzi wa soka nchini walivyozoea kumwita.

Sunday baada ya kucheza soka kwa mafanikio hapa nchini, mwaka 1976 alitimkia nchini Uholanzi katika klabu ya Heracles akiwa mtanzania wa kwanza kucheza soka la kulipwa Ulaya na alikaa na klabu hiyo hadi 1978.

Mwaka 1979 alikwenda Marekani kucheza soka la kulipwa katika klabu ya New York Eagles ambayo alikaa nayo mwaka mmoja na kutimkia klabu ya Australian ya Australia mwaka 1980.

Mwaka 1981 alikwenda Dubai kujiunga na klabu ya Al-Nasri iliyokuwa miongoni mwa timu timu kubwa kwenye Ligi Kuu nchini Dubai kabla ya kurejea nyumbani 1984 na kuamua kustaafu kucheza soka ya ushindani.

Nyota huyo ambaye alichezea kwa mafanikio timu ya Yanga, Pan African
na timu ya taifa, Taifa Stars, kabla ya kwenda Ulaya kucheza soka la kulipwa, akiwa na timu hizo alikuwa anaonesha uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu, hali iliyosababisha wapenzi na mashabiki wa Yanga kumbatiza jina la ‘Computer’ hesabu kwa haraka sana.

Wakati huo Sunday akipachikwa jina hilo, teknolojia ya mashine hiyo ilikuwa bado haijaingia nchini na watu wengi walikuwa hawaijui na wala kuiona, lakini nyota huyo kutokana na uhodari wake, wepesi na uwezo mkubwa wa kupachika mabao alibatizwa jina hilo.

Sunday alianza kucheza soka akiwa na timu za mitaani katika miaka ya 1960 mwishoni na baadaye katika miaka hiyo kutokana na kuonesha uwezo mkubwa wa kucheza soka alichukuliwa na kikosi cha Yanga B.

Akiwa na kikosi cha Yanga B, kutokana na umahiri mkubwa aliokuwa akiuonesha katika kusakata soka mwaka 1969, alisajiliwa rasmi kuchezea kikosi cha wakubwa yaani Yanga A, huku akichezea safu ya kiungo mshambuliaji namba nane.

Pamoja na kucheza safu hiyo, lakini wakati mwingine alikuwa akipangwa kucheza winga ya kulia, sentafowadi, kumi na hata winga ya kushoto, kwani namba zote hizo alikuwa na uwezo wa kuzicheza.

Kadiri siku zilivyozidi kusonga mbele, Sunday akawa ni mmoja wa wachezaji wa kutumainiwa wa klabu hiyo na akawa ni miongoni mwa wapachikaji mabao wakuu, huku akiwa kipenzi mkubwa wa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo yenye maskani yake makuu mtaa wa Jangwani na Twiga.

Agosti 10, 1974 katika ligi ya Taifa (sasa Ligi Kuu), katika mchezo wa mwisho Yanga wa Nyamagana, mjini Mwanza, Yanga ilishinda mabao 2-1, huku Sunday akifunga bao la pili katika dakika ya 97.

Mechi hiyo ambayo inachukuliwa kama ni ya kihistoria kwa timu hizo zilipokutana, katika dakika 90 za kawaida matokeo yalikuwa ni sare ya bao 1-1 na baada ya hapo ndipo walipoongeza dakika 30 za nyongeza kusudi mshindi apatikane.

Katika mechi hiyo bao la kusawazisha la Yanga lilifungwa na Gibson Sembuli (marehemu), dakika tatu kabla ya mchezo kumalizika yaani katika dakika ya 87, huku bao pekee la Simba lilifungwa na Adam Sabu ambaye pia ni marehemu katika dakika ya 16.

Pia mwaka huo huo wa 1974, Sunday alikuwa katika kikosi cha timu ya Taifa Stars, kilichotwaa Kombe la Chalenji, michuano iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam (sasa Uhuru).

Mwaka 1975 katika fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati Yanga dhidi ya Simba, mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar, Yanga walibuka na ushindi wa mabao 2-0, huku Sunday akifunga bao la kwanza na Sembuli akifunga bao la pili.

Mwaka huo wa 1975 kutokana na uwezo, kipaji kikubwa alichokuwa akikionesha na hasa baada ya kuifungia timu hiyo katika mchezo wa Nyamagana na ule wa Zanzibar, ndipo wapenzi na mashabiki wa Yanga walipombatiza jina la Computer wakimfananisha na mashine hiyo inayopiga hesabu kwa haraka sana.

Baada ya nyota huyo kupachikwa jina hilo lilivuma na kuzoeleka mno na wapenzi wa soka nchini hususan wa klabu ya Yanga hadi alipoamua mwaka 1984 kustaafu kucheza soka ya ushindani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -