Thursday, November 26, 2020

SVEN APIGA HESABU KUKAA KILELENI VPL NA ONESMO KAPINGA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck, amesema anaamini kikosi chake kitaendelea kufanya vyema Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) na kukaa kileleni.

Simba ilifanikiwa kupata ushindi wa tano, baada ya kuifunga mabao 5-0 Mwadui katika mchezo wa ligi hiyo uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Kabla ya ushindi huo, Simba ilipoteza michezo miwili mfululizo ikifungwa bao 1-0 na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga, kisha kupata kichapo kama hicho kutoka kwa Ruvu Shooting katika dimba la Uhuru.

Akizungumza baada ya mchezo wa juzi dhidi ya Mwadui, Vandenbroeck alisema amefurahi kupata ushindi huo, baada ya kuwa katika wakati mgumu wa kupoteza pointi sita ugenini na nyumbani.

Vandenbroeck  alisema  katika mchezo huo katika kipindi cha kwanza wapinzani wao walionesha upinzani na kujikuta wakienda mapumziko wakiwa mbele kwa mbao 1-0.

Alisema kikosi chake kilifanikiwa kuondoka na ushindi baada ya kufanya mabadiliko ya wachezaji katika kipindi cha pili na baadaye kupata mabao mengi.

Kocha huyo alisema baada ya ushindi huo, ataendelea kuboresha kikosi chake kutokana na kasoro zilijitokeza ili kuhakikisha wanapata ushindi katika michezo itakayofuata.

Alisema malengo yake ni kuongoza katika msimamo wa ligi hiyo na baadaye waweze kutetea ubingwa wao kwa mara ya nne mfululizo.

Katika mchezo huo, mabao ya Simba yalifungwa na John Bocco aliyefunga mawili, Hassan Dilunga Ibrahim Ajibu na Said Ndemla.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -