Thursday, November 26, 2020

Sven aruka kihunzi

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ASHA KIGUNDULA

KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na Muzamiru Yassin baada ya sare ya bao 1-1 na Yanga juzi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, Simba walizidiwa kipindi cha kwanza kabla ya kuzinduka kipindi cha pili na kuwatesa mno Yanga.

Pongezi ziendea kwa Sven kwa kufanikiwa kuwasoma Yanga kabla ya kuja kivingine kipindi cha pili na kujisafisha mbele ya mashabiki, wanachama na viongozi wa timu hiyo.

Ikumbukwe kuwa kabla ya mchezo, Simba walikuwa na matarajio makubwa ya ushindi wakiamini kuwa na kikosi bora, zaidi wakiringia ubora wa Chama na nyota wengineo wa timu yao.

Lakini kutokana na jinsi walivyozidiwa na Yanga, hasa kipindi cha kwanza, watu wa Simba wanaamini kuna wachezaji wao, hasa Chama, hawakuwajibika ipasavyo.

Akizungumza baada ya mchezo huo, mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Zacharia Hansppope, alisema kuwa Chama hakucheza katika kiwango chake, akionyesha kuwa na wasi wasi naye.

Mbali ya Chama, nyota wengine wa Simba walioshikwa ‘uchawi’ baada ya mchezo wa juzi jioni ni Muzamiru, Rally Bwalya na Jonas Mkude.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa wachezaji hao, Sven yeye ameonekana kuwa salama ikionyesha wazi kazi yake kukubalika.

Na kati ya vitu vilivyomwokoa kocha huyo, ni kitendo cha kuutumia vema muda wa mapumziko kuwaelekeza wachezaji wake jinsi ya kuwamudu Yanga na kweli wakafanikiwa katika hilo.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Sven alisema kuwa baada ya sare hiyo ya juzi, anakwenda kujipanga upya kwa ajili ya mechi zao zijazo.

Alisema walikuwa wakitambua kuwa wapinzani wao wamejipanga kupata matokeo kama walivyopanga wao, hivyo mkakati wao ilikuwa kupata pointi zote tatu lakini haikuwa hivyo.

Alisema amewapa wachezaji wake mapumziko mafupi kupisha michuano ya kuwania Fainali za Mataifa ya Afrika, timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, nayo ikishirki. 

“Licha ya kukosa baadhi ya wachezaji wangu kutokana na kuwa majeruhi, wengine wote walikuwa kwenye hali ya mchezo, yameshatokea, sasa tunajipanga kwa ajili ya mechi zijazo,” alisema Sven.

Bao la Yanga juzi lilifungwa na Michael Sarpong dakika ya 29 kwa mkwaju wa penalti kabla ya Simba kusawazisha dakika ya 86 kupitia kwa beki Joash Onyango.

Simba inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, ikiwa na pointi 20 baada ya kucheza mechi 0, ikitoka sare mechi mbili, kufungwa mbili na kushinda sita.

Yanga wao wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 24 baada ya kucheza mechi 10, wakishinda saba na kutoka sare mechi tatu, huku Azam wakiwa kileleni na pointi zao 25, wakishinda mechi nane, sare moja na kufungwa moja.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -