Thursday, November 26, 2020

Sven atoa kali, akimbilia TFF

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

 NA WINFRIDA MTOI

HOMA ya pambano la watani wa jadi imezidi kupanda baada ya Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, kushindwa kulizungumzia na kukimbilia Shirikisho la SokaTanzania(TFF) kuwa ndipo atakapotolea ya moyoni.  Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara unatarajiwa kupigwa kesho kwenye dimba la Mkapa, jijini Dar es Salaam. Sven licha ya kusema hana wasiwasi, lakini alishindwa kuzungumzia mtanange huo mbele ya waandishi wa habari baada ya mchezo na Kagera Sugar walioshinda 2-0 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. “Nafurahia kiwango kizuri cha wachezaji wangu walichoonesha kwa Kagera Sugar, mechi ya Yanga siwezi kuizungumzia, ina sehemu yake ni TFF, tukikutana makocha  wa timu zote kuzungumza Ijumaa(leo),” alisema Sven. Katika hatua nyingine mashabiki wa Simba wameonekana kula  kiapo  wakisema Yanga hatoki kutokana na kukamilika kwa kikosi chao. Mashabiki hao walianza tambo juzi baada ya kuichapa Kagera Sugar, huku wakitambia  aina ya soka lao walilolipa jina la pira biriani. Baadhi ya wapenzi hao wa Simba, walifika uwanjani wakiwa na sahani za biriani na kula hadharani baada ya mechi na kusema ni salamu kwenda kwa watani wao Yanga. Mashabiki hao walionekana mwenye mzuka wakitamani siku ya mechi hiyo, inayosubiriwa kwa hamu ifike haraka wakiamini ushindi upo wazi. Wanamsimbazi hao walitamba kuwa tayari wamepunguza pointi walizokuwa wamepitwa na Yanga, hivyo nne zilizobaki tatu watachukua Jangwani. Miongoni mwa mashabiki hao walitoa tambo zao anajulikana kwa jina la Mzaramo wa Simba, alisema ushindi ni kawaida yao, mechi mbili walizofungwa waliteleza bahati mbaya. “Tumeshaanza sherehe, sisi wazaramo tunasema tumeanza biga, kama kuloeka mtama na vitu nyingine, Jumamosi tunaamkia shughuli ya kumtoa mwali. “Kitakachomfika Yanga hakuna wa kumuombea, tunasema mashabiki wote wa Simba waje uwanjani kwa furaha kabisa ili tuchukue pointi zetu,” alitamba Mzaramo wa Simba. Shabiki mwingine wa Simba maarufu kwa jina la Big, aliyetinga uwanjani akiwa na jogoo mkononi, alisema maandalizi ya biriyani yameanza, hawana wasiwasi. “Nataka niwaambieje ndugu zetu, kama wanajua Chama(Clatous), wameumia wao, sisi hatuna mambo mengi bali tukutane uwanjani,” alisema Big.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -