Sunday, January 17, 2021

TABIA HII HAICHOCHEI MAPENZI ZAIDI YA KUMALIZA NGUVU YAKO KWA MWENZAKO

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA RAMADHAN MASENGA

KILA muda unataka kuwa karibu na mwenzako. Hutaki atoke peke yake, hutaki awe huru na simu yake. Unataka kokote aendapo uwe naye. Unataka chochote afanyacho ujue. Uko hivyo?

Sawa. Kwa wengi kufanya hivi ni njia ya kudhibiti wapenzi wao dhidi ya usaliti. Wana amini wakiwaacha ‘huru’, wawe tayari kufanya lolote itakuwa hatari kwao. Kwamba wanahisi watasalitiwa.

Japo wengi wanadhani hivyo, ila tafiti za kitaalamu zinasema tofauti. Tafiti zinaonesha kuwa japo kuwa sambamba na mpenzi wako kunaweza kusiwe na madhara makubwa sana, ila kumpa mwenzako nafsi ni njia sahihi ya kuchochea upendo kwa mwenzako.

Iko hivi. Ili mtu awe na shauku sana na kitu inabidi awe nacho muda fulani na akikose muda fulani. Yaani kitaalamu ili mtu awe na shauku na hamu zaidi na wewe, kuna wakati inabidi uwe kama ‘unampotezea’ hivi. Hali hii itasababisha mwenzako awe na shauku na kiu zaidi na wewe.

Ili kupata uelewa wa kutosha zaidi wa suala hili angalia mfano huu kwa makini zaidi. Kupitia mfano huu utapata kitu unachotakiwa kukipata.

Unaweza kuwa unapenda sana wali. Kwa kupenda kwako wali utapenda sana kula chakula hiki. Ila japo ukweli uko hivi, ila mapenzi yako kwa wali yanaweza kufubaa (wear off) kama kila muda utakuta chakula hicho mezani. Yaani baada ya kula na kuridhika ila bado chakula kipo katika masufuria, mezani na kwenye makasha ya kuhifadhia chakula.

Japo bado chakula hiki utakuwa unakipenda sana ila hali hii itafanya usiwe na ‘ubabaiko’ tena na chakula hiki kama ilivyokuwa mwanzo.

Na kwa mpenzi wako pia hali iko hivi. Kuna wakati inabidi ujitoe kwa mwezako ili afurahie na ajivunie kuwa na wewe. Ila kuwa makini na hali hii. Ukijiachia sana kwa mwenzako, ukamnyima fursa ya kukaa mwenyewe na kutafakari masuala mengine, ukambana sana kuhusiana na simu yake, unafubaa katika maisha yake. Epuka hali hii.

Kumbana mwenzako si njia ya kumfanya asikusaliti. Kumbana mwenzako kutamfanya mwenzako akuone wa ‘kawaida’ sana na kushindwa kufurahia sana na wewe.

Tambua mapenzi ni suala la kuwa makini na mwenzako na kujua namna ya kucheza na akili yake. Utamdhibiti mwenzako ukiweza kudhibiti akili yake. Yaani umfanye akuone bora, wa kipekee na wa thamani sana. Huwezi kumdhibiti mwenzako kwa kumzua asitoke nje. Huwezi kumdhibiti mpenzi wako kwa kuchunguza sana simu yake.

Sababu ya mwenzako kwenda nje inaanzia katika akili na kisha hisia zake. Sasa yanini ujichoshe kudhibiti mwili wake wakati unaweza kupambana na akili yake na kufanikiwa kumaliza mchezo?

Ili mwenzako umteke si suala la kumzuia asitoke ama asiwasiliane na fulani. Ila ni suala la kumfanya akutafsiri vema, akuone bora na aamini wewe ndiyo faraja na raha halisi ya maisha yake. Na moja ya njia ya kukamilisha mchakato huu vizuri, ni kumpa nafasi.

Mpe nafasi mwenzako. Mtu huwa mjinga maradufu kwa kitu ambacho hakimgandi. Angalia mfano huu mwingine. Unaenda dukani kununua nguo. Unaona nguo nzuri na kuulizia bei. Muuzaji anataja bei ambayo ni kubwa kuliko kiwango cha pesa ulichobeba. Unaanza kuhangaika kuomba akupunguzie bei.

Unafanya hivi si kwamba nguo hii ni nzuri na bora zaidi kuliko zote ulizo nazo kabatini, hapana. Unafanya hivi kwa kusukumwa na umbali wa nguo hii na zile ulizonazo nyumbani. Za nyumbani hazikubabaishi sana kwa sababu kila ukigeuka zipo, kila dakika unaziona.

Hata kama umeoa ama kuolewa mfanye mwenzako akutamani kwa kumpa nafasi ya kufanya mambo yake na biashara zake. Hii haimaanishi uache kumpigia simu ama kumwandikia sms akiwa kazini, hapana. Hii inahusisha kuacha kumbana mno mpaka akuone kero. Mwenzako hafai kukuona kero. Mwenzako ili akupende na akuone bora zaidi ni lazima akuone wewe ndiye chanzo cha raha na burudani katika maisha yake.

Kuna wakati inabidi uwe tofauti kwa mwenzako. Akuone na hali tofauti (mood) na uzungumze mambo ambayo mengine hajawahi kusikia ukizungumza. Yote unafanya katika kujenga upya katika akili yake.

Watu wengi wanakosea kudhani kujiweka karibu sana na wandani wao hata kuwazuia kufanya mambo mengine ni bora sana. Nakwambia si bora sana. Ukiendekeza kufanya hivyo unajifubaisha kwa mwenzako.

Mapenzi ni suala la namna mwenzako anavyokutafsiri katika akili na hisia zake. Kama anakuona upo upo tu, mtu ambaye kama ilivyo jana pia upo hivyo hivyo hata leo. Hali hii itampunguzia hamasa kwako.

Jiweke tofauti. Mpe nafsi mwenzako katika mambo na harakati zake. Hii itamtia njaa juu yako pamoja na hali ya yeye kutojiamini sana kwako.

Kuna wakati mwenzako hatakiwi kujiamini sana kwako. Inabidi awe na punje ya mashaka kwamba akicheza tu utadakwa na mwingine. Hii itamfanya ajitulize kwako na kuwa tayari kukufurahisha kwa mambo na vitu unavyotaka.

Kusema awe na mashaka haimaanishi ufanye vitu vya kijinga vya kumtia wasiwasi. Hapana. Inabidi namna unavyojiweka, ulivyo bora kwake, unavyomfurahisha kumfanye akose kujiamini sana hata aone kwamba wewe ni bora sana kiasi ajione kukupata kwake ni bahati.

Mwandishi wa makala hii ni mtaalamu mbobezi wa masuala ya ushauri wa uhusiano, maisha na utulivu wa hisia (Psychoanalyst).

ramadhanimasenga@yahoo.com

Previous articleNILISHAKUFA
Next articleGARI LIMEWAKA
- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -