Thursday, October 22, 2020

TAIFA STARS VS UGANDA MASHABIKI WAINGIE BURE U/TAIFA

Must Read

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

NA WINFRIDA MTOI

HABARI kubwa inayozungumzwa kwa sasa ni ushindi wa timu ya Tanzania, Taifa Stars dhidi ya Cape Verde uliopatikana katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam juzi.

Taifa Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu fainali za Afrika (Afcon), zitakazochezwa mwakani nchini Cameroon.

Ushindi huo uliibua furaha kwa Watanzania baada ya timu yao  kufungwa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Cape Verde.

Matokeo hayo yameiwezesha Tanzania kushika nafasi ya pili katika Kundi L, kwa pointi tano kabla ya jana Lesotho kucheza na Uganda ambao wanaongoza kwa pointi saba.

Katika mchezo wa juzi, mashabiki  wengi walijitokeza kwenye Uwanja wa Taifa kwa lengo la kuhamasisha ushindi  hasa baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 3-0 na wapinzani wao.

Kama ilivyokawaida kuwa shabiki ni mchezaji wa 12 uwanjani, imedhihirika juzi kutokana na kikosi cha Stars kuonekana kuwa na nguvu tofauti na walivyocheza ugenini.

Kwa kutambua mchango wa mashabiki uwanjani, hivi karibuni Serikali ya Kenya iliamua kutangaza kiingilio bure katika mchezo wa timu yao ya Taifa dhidi ya Ethiopia na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Ni wazi, idadi kubwa ya mashabiki uwanjani ambao hushangilia kwa nguvu ni moja ya mbinu inayoweza kumaliza mpinzani kwa sababu inawapa wachezaji  ujasiri wa kushinda.

Hali hiyo imedhihirika juzi pale kwenye Uwanja wa Taifa kwa jinsi mashabiki wa soka walivyojitoa kuishangilia timu yao bila kujali kama walipoteza mchezo uliopita.

Kitendo cha mashabiki hao kujaa uwanjani, haikuchangiwa na kitu kingine bali kiingilio cha chini ambacho kilikuwa Sh 2000 kwa mzunguko na Sh 10,000 kwa VIP.

Awali Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lilitangaza kiingilio cha chini Sh 5,000, lakini baadaye kilianza kulalamikiwa kutoka kwa baadhi ya wadau wa soka hasa baada ya kubaini nchi jirani kama Kenya iliruhusu mashabiki kuingia bure ili kusapoti timu yao.

TFF walisikia kilio cha mashabiki na kuweza kupunguza kiingilio hicho.

Ikumbukwe kuwa baadhi ya michezo ya Stars ya nyuma hasa baada ya timu kutoka kupata matokeo mabaya, mashabiki walikuwa wakijitokeza wachache lakini juzi umati ulikuwa ni mkubwa sana ukizingatia ilikuwa siku ya kazi.

Umati ule uliofika kuisapoti Stars, ulimpa nguvu pia hata kocha wa kikosi hicho, Emmanuel Amunike na kutambua ana deni la kuhakikisha anawafurahisha Watanzania walioacha shughuli zao na kwenda uwanjani.

TFF watambue mwitikio ule ni kiingilio cha Sh 2000 walichoweka, hivyo kuna haja ya kuendelea na utaratibu huo katika michezo mingine ya timu ya taifa ili kuwapa nafasi Watanzania kuwapa sapoti wachezaji wao.

Hakuna asiyependa kuishangilia timu yake ya Taifa, bali kikwazo  kimeonekana wazi juzi kuwa ni viingilio vilivyokuwa vikiwekwa ambavyo wengi walikuwa hawana uwezo wa kuvimudu.

Nina imani na shirikisho pamoja na  washirika wake kwamba suala hilo waliangalie zaidi ili kuwawezesha mashabiki wakiwamo wa mikoani kuvutika kufika Dar es Salaam kushangilia timu yao.

Bado sapoti ya mashabiki kwa Stars inahitajika ili iweze kufuzu fainali za Afrika, ukizingatia michezo iliyobaki ni miwili, mmoja ugenini na mwingine nyumbani dhidi ya Uganda.

Naamini itakapofika mechi na Uganda, kiingilio kiwe Sh 2000 au mashabiki waingie bure kwa lengo la kuwapa hamasa wachezaji, ikizingatiwa mchezo huo utakuwa ni muhimu kushinda ili kuweza kufuzu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na Staa Wako, safu inayokupa nafasi...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -