Saturday, November 28, 2020

‘TAJIRI WA MAHABA’ ALIVYOWAPA THAMANI MAKUNGWI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA,

TAJIRI wa mahaba ndilo jina alilopewa na mashabiki wake baada ya kuwa gwiji wa nyimbo za mapenzi hasa baada ya kuanza kazi hiyo rasmi.

Jina alilopewa na wazazi wake ni Kassim Maganga ambaye takribani asilimia 99 ya nyimbo anazoziimba  zinakuwa zina ujumbe wa mapenzi.

Kassim Mganga tajiri asiye na fedha ila mwenye milki kubwa ya utajiri wa mahaba, ameamua kutumia uwezo wake wote kuonyesha kipaji chake cha kutunga na kuimba vema nyimbo za mapenzi.

Ni mmoja kati ya vijana walioingiza ladha tofauti kwenye muziki wa bongo fleva na msanii mwenye nidhamu anapokuwa katika maisha ya kawaida.

Ndiye yule msanii aliyeimba, ‘Nakuimbia’, kisha Awena halafu akaimba ‘Haiwezekani’, ‘Tajiri wa Mahaba’, ‘Amore na I love You; zote hizo huzitoa kwa nyakati tofauti.

Umaarufu alioupata kwenye nyimbo hizo ndio umempa nguvu ya kuendelea kutoa nyimbo kali za mapenzi ambapo kwa sasa anatamba na kibao chake kipya cha Somo.

Wimbo huo wa Somo ndiyo habari ya mjini kwa sasa; kwenye pub, klabu, bodaboda, bajaji, redioni na simu za mkononi ni ‘Somo, Somo, Somo’.

Ni kibao kilicho katika miondoko ya pwani, hasa chakacha na mashairi yake kufundisha na sauti ya kuburudisha ambayo imenogeshwa na mkongwe Nyota Waziri.

Kufuatia kufanya vema kwa wimbo huo, BINGWA inauchambua wimbo huo huku ikizungumza machache na Kassim Mganga ambaye kwa sasa ananogesha Bendi ya Kilimanjaro.

Alivyompa thamani Somo/Kungwi

Somo imebeba ujumbe wa sifa njema kutoka kwa mwanamume aliyeoa kwenda kwa kungwi au mwalimu aliyemfunda mke. Kassim Mganga ameoa mwanamke anayeyajua mapenzi, hivyo anarudisha shukrani kwa kungwi/somo.

Ndani ya wimbo huo, Kassim amemmwagia sifa somo ambaye ni Nyota Waziri kwa kuweza kumtengeneza vema mke wake ambaye amekuwa akimuonyesha mapenzi ya dhati.

Mashairi ya wimbo huo yamekuwa yakimzungumzia somo, jambo ambalo limeonekana kuwapa thamani wale wote wanaowafunda wari kwa nyakati tofauti.

Lakini pia kwenye wimbo huo kanga imepewa hadhi ya kupendezesha sehemu nyingi kama zilivyoonekana kwenye video hiyo, huku Nyota Waziri Naye akitupia Kiafrika zaidi.

Alipoanzia

Kassim Mganga alizaliwa kwenye familia ambayo alikuta baba ni mwanamuziki na mama anaimba, akakulia katika familia ya wanamuziki na hivyo akaanza taratibu kuwa mwanamuziki.

Baba yake, Hemed Salim Mganga alikuwa bendi ya Legho Stars na mama akiimbia vikundu vya Bandari Modern Taarabu ya Moni Tanga na Coast Modern Taarab.

Alianza kuimba pamoja na baba yake kweye bendi ya Legho Stars kabla ya kukutana na Dj Muli B, baada ya kutoa wimbo wa Haiwezekani katika studio za Komorir na kujikita rasmi kwenye bongo fleva mwaka 2007.

Kwanini tajiri wa mahaba

Nyimbo zake za Awena, Usiende kwa Mganga, Subira na nyinginezo ndizo zilizomfanya kutamba kwamba yeye ndio fundi au tajiri wa nyimbo za mahaba.

Ujuzi wake wa kutunga mashairi, kuandika na kutengeneza melody nzuri ndizo zimemfanya jina hilo kukubalika hata na wale mashabiki ambao awali walipinga vikali jina hilo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -