Sunday, October 25, 2020

TAJIRI WA MASIKINI – 10

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA EMAN FISIMA


 

Ilipoishia

Watu wengi walikuwa wakiendelea kuteseka na kuishi maisha ya shida kama vile walikuwa wakimbizi, maana wao hawakuweza kuuza mazao yao jijini Port Villa na kwingineko. Wengine hawakuweza kufanya kilimo rahisi kwa sababu hawakuwa na pampu za maji, hivyo waliishi kwa kilimo kidogo kisicho na hata tija ndogo.

Watoto walikufa sana kwa ugonjwa wa utapiamlo, malaria sugu,  kipundipindu na maradhi mengine yatokanayo na kuishi maisha ya uchafu. Karibu kila siku nyumbani kwangu walikuwa wakija watu kuniomba msaada wa chakula na nguo,  kwa kuwa mimi ndiye niliyekuwa kijana pekee mwenye uwezo yaani tajiri wa masikini, nilijitahidi pale nilipoweza.

Roho yangu ya huruma na mapenzi kwa watu wa kabila langu, ndio vilivyonifanya nijivute niwezavyo kuwasaidia baadhi ya watu walioshindwa kabisa kusogea hata hatua mbili. Wasichana wengi walikuwa wakiitumia miili yao kulisha familia zao kwa kujiuza kwa wanaume kutoka Port Villa naweza kusema hiyo ndio biashara iliyokuwa ikiwainua wengi kutoka kwenye njaa kali.

*********

Nilidhani majibu ya mke wangu kwa Franco Mazimbe yangemfanya kijana huyo aache kumfuata mke wangu, nilidhani yangemfanya asije kuivunja ndoa yangu lakini kumbe ilikuwa sivyo. Franco alianzisha njama za kunidhoofisha mimi kiuchumi ili aweze kumpata mpenzi wake wa zamani yaani mke wangu kipenzi.

Alianza kupeleleza juu ya maisha yangu, akitaka kujua kwanini nilikuwa nikiyamudu maisha kuliko vijana wote wa vitongoji vya Adorra na Katanga. Lengo lake lilikuwa ni kuniyumbisha ili mke wangu Rumia anikimbie na kwenda kwake.

SASA ENDELEA…

Alipata habari kuwa maisha yangu yalikuwa yakitegemea kilimo cha mboga na matunda, kwa uwezo wa pampu iliyokuwa ikivuta maji kutokea Mto Vuma. Hakujali sana jambo hilo alichojali yeye ni njia gani nilizokuwa nikizitumia kusafirisha mazao na kupata kibali cha kuyauza jijini kwao Port Villa.

Hapo ndipo alipoumiza kichwa kwa sababu alifahamu kuwa ilikuwa si rahisi kwa Mpache kupata soko la mazao au bidhaa yake yoyote katika maeneo na masoko mbalimbali katika miji inayokaliwa na wao hasa Port Villa. Alijiuliza mimi nilikuwa nimewezaje, ilibidi afanye utafiti wa kujua nilikuwa nafanikisha vipi biashara hiyo katika jiji lao. Yote hiyo ilikuwa ni kutaka kunifanya nisiweze kuyamudu maisha ili apate nafasi ya kumrudisha mpenzi wake wa zamani, kipenzi mke wangu Rumia.

Nikiwa sina hili wala lile, alikuwa amewatuma watu kunipeleleza, kuanzia ninapovuna mazao yangu hadi ninapoyapakia kwenye gari la kukodi na kuyapeleka jijini Port Villa.

Alipewa taarifa na watu wake pia kuwa biashara yangu hasa ilimtegemea mtu mmoja aliyeitwa Rahimu Mhai mwenzao aliyekuwa akiniwekea mazao yangu kwenye eneo lake katika soko kuu la jijini Port Villa.  Alijua kuwa mtu huyo ndiye aliyekuwa kila kitu kwangu.

**************

Licha ya ubaguzi, watu wa Port Villa au Wahai walikuwa hawapendi kununua mazao kwetu kutokana na kuhisi kuwa wangekula vyakula vichafu vilivyolimwa kwenye mazingira hatarishi, kwa sababu vitongoji vya Adorra na Katanga vilikuwa na mazingira duni na machafu kutokana na miundominu yake kuwa mibovu. Walikuwa wakihisi kuwa chembechembe ndogo za maji ya viwandani zilikuwa zikiingia kwenye Mto Vuma.

Franco Mazimbe aliwatafuta watu kama 10 hivi, akiwalipa kwa kazi moja. Watu hao walikwenda kwa nyakati tofauti kununua matunda na mboga zangu katika eneo la Rahimu. Baada ya siku mbili kila mmoja alirudi na malalamiko yake katika eneo la Rahimu, akilalamika kuuguliwa na tumbo, wengine walikuja na watoto wao, watoto hao nao walidai kuwa walianza kusumbuliwa na matumbo mara baada tu ya kula matunda yangu.

Siku hiyo wakati watu tofauti wakija hapo sokoni, nami nilikuwepo kusimamia biashara yangu. Watu hao walisema wanasumbuliwa na matumbo hayo kutokana na kula mboga na matunda yaliyouzwa katika eneo la Rahimu. Ilikuwa ni siku baada ya siku watu tofauti walikuwa wakija kulalamika eneo hilo na kusababisha watu kujaa na kumtazama Rahimu aliyekuwa haelewi. Mimi naye niliyekuwa huko kwa siku tano, nilishwangazwa na watu kuumwa na matumbo kutokana na kula mazao yangu.

Polisi walifika eneo la Rahimu na kutuhoji wote wawili, wakitaka kujua matunda na mbogamboga hizo zilikuwa zikitokea wapi. Wakati tukihojiwa na polisi, uongozi wa soko pia ulikuwepo kuhakikisha unatambua tatizo hilo. Baadhi ya wafanyabiashara katika soko waliokuwa wakinifahamu kuwa mimi ni Mpache kutokea Adorra, niliyekuwa nikileta mazao hapo na kusaidiwa na Rahimu waliongeza uchochezi wa suala hilo la watu kuugua matumbo.

Mtu mmoja alisema jambo hilo lilitakiwa kufikishwa kwa mabwana afya ili wafanye utafiti wa kutambua kama mboga na matunda hayo yalikuwa salama kwa kuliwa. Saa chache zijazo walikuja watu sita waliojiita mabwana afya wakiongozwa na afisa usafi wa soko kuu na kuzichukua mboga hizo na kwenda kuzifanyia uchunguzi.

Hakika mimi nilizidi kuchanganyikiwa sikuelewa jambo lolote, nilibaki nikimtazama Rahimu ambaye naye akiwa haelewi jambo lolote. Rahimu aliniuliza kuwa  mbona yeye na familia yake wamekuwa wakila mboga na mtunda yangu karibu kila siku na  hawaumwi na matumbo wala kusumbuliwa na kitu chochote?

Nilimtazama tu kwa sura ya huzuni na mimi nilijibu.

“Hata mimi sielewi ndugu yangu, kwa sababu familia ya nyumbani kwangu, mama wadogo zangu, wanakula mboga na matunda haya, hata siku moja sijawahi kuona wakilalamika na maumivu ya matumbo. Pia mimi na mke wangu kila siku tunatumia, hatujawahi kuharisha wala kuugua homa yoyote ya matumbo, hakika nawashangaa sana watu hawa.”

Tukiwa bado pale sokoni, polisi wakiwepo na watu wengine wasionipenda mimi kama Mpache, wakiwa wametuzunguka, wale mabwana afya na ofisa wa soko waliokwenda kuzifanyia uchunguzi mboga na matunda yangu, walirudi na majibu yao. Walisema kuwa mboga hizo hazifai  kwa chakula  kwa sababu zilikuwa na chembechembe ndogo za kemikali zitokanazo na maji ya viwandani.

Mimi na Rahimu tulibaki midomo wazi, mwili wangu ulianza kutetemeka, upesi niliwaambia.

“Sio kweli wakuu kwa sababu maji ya viwandani yanakwenda sehemu nyingine na yako mbali na Mto Vuma.”

Bwana afya mmoja aliniambia.

“Si unalima pembezo mwa mto? kumbuka unatumia udongo ambao umeanzia kulea maji ya viwandani  yaliko, hivyo lazima chembechembe za kemikali ziingie kwenye mazao.”

Nilihema kidogo nikamtazama Rahimu na kusema.

“Hapana, mimi shamba langu la mazao liko mbali na mto ni kama kilomita moja hivi, situmii udongo wa pembezoni mwa mto.”

“Pamoja na hayo kijana, lakini maji unayotumia si ya mto huo? kwa sababu kwa mujibu wa utafiti wa kitaalamu, maji husafirishwa na udogo hivyo ule unyevunyevu unaobeba kemikali hutembea hadi kwenye udogo wa pembezoni mwa mto na kujichanganya na udongo wake ambao baadaye huingia katika maji. Kwa hiyo maji unayovuta ndio hayo unakwenda kumwagilia mboga na matunda yako,” aliongea mtu mwingine aliyekuwa na faili pamoja na kalamu.

Nilitambua kuwa jambo hilo haliwezakani kwa sababu kiwanda kilikuwa mbali sana na mto na pia mimi nilikuwa nikilimia  mbali sana na mto Vuma, ingawa sikusoma shule ya sekondari wala chuo, lakini nilijua tu kuwa mabwana afya hao hawakuwa wakweli.

Lakini kwa kuwa nilikuwa mtu wa kutoka kitongoji masikini, adui wao wa ubaguzi, nilikuwa naona dalili za kushindwa kabisa, hapo ndipo nilipokuwa nikizidi kuchanganyikiwa.

Mabwana afya hao wakishirikiana na Polisi pamoja na uongozi wa soko, waliamuru kuwa kuanzia siku hiyo nisilete mazao yoyote kutoka Adorra au Katanga, kauli hiyo ilinipa mshtuko mkubwa sana.  Askari polisi mmoja alimsogelea Rahimu na kumwambia.

“Endapo kijana huyu ataleta mazao tena katika sehemu yako ya soko, wewe ndio utabeba tamu zake, tutakufikisha mahakamani kwa kosa la kuwalisha watu mboga chafu zenye kemikali.”

Nilishuka chini kama mtumwa na kuwapigia magoti watu hao nikiwasihi wasichukue uamuzi huo, niliwahikishia kuwa mazao yangu hayakuwa na kasoro yoyote.  Niliwaambia kwa nidhamu ya hali ya juu kuwa maisha yangu yalikuwa yakitegemea biashara hiyo, familia yangu na ndugu zangu wote walikuwa wakiishi kwa biashara hiyo.  Lakini hakuna aliyenisikiliza zaidi askari polisi mmoja alinisogelea na kuniambia.

“Kijana unajua hivi sasa ulitakiwa uwe polisi kwa kosa la kuwalisha watu vyakula vyenye sumu? Sasa usitake tukupeleke mahakamani, maana ukifikishwa kwa korti kifungo chake kinaweza kuwa miaka 10, maana hilo ni kosa kubwa la jinai. Tumekusamehe kwa kuwa ulikuwa hulijui hilo.”

Nilibaki nikimtazama tu askari huyo huku nikigeuza shingo yangu ya huruma, nikimtazama Rahimu aliyekuwa akishindwa kunitetea. Watu wengine waliokuwa hawataki kuniona pale sokoni nao walibaki kushangilia katika mioyo yao. Rahimu alibaki akinitazama kwa huruma maana yeye mwenye aliogopa kufikishwa  mahakamani au kuhatarisha biashara yake pale sokoni.

Mabwana afya na askari polisi  walipoondoka pale sokoni, nilibaki mimi na Rahimu, nilikaa chini kwa uchovu, nikihisi kichwa changu kikiwaka moto, mwili wangu ulitetemeka nilijihisi dunia yote imenilemea mimi na inataka kunizika kabisa, maana sikuona msaada wowote utakaojitokeza mbele yangu.

Nini kitaendelea? Usokose kesho

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -