Wednesday, October 21, 2020

TAJIRI WA MASIKINI (14)

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA EMAN FISIMA      |      


 

Ilipoishia

Rumia alizidi kuona tofauti yangu na unyonge wangu, naye alianza kuingiwa na wasiwasi.  Siku ya pili alishangaa kuona sijaenda shambani kama ilivyo kawaida ya siku zote. Kawaida ilikuwa nikipumzika Jumapili tu lakini siku hiyo ilikuwa Jumatano.  Aliponiuliza nilimwambia kuwa napumzika kwa sababu nilikuwa nimefanya sana kazi pindi nilipokuwa jijini Port Villa.

Alinielewa kwa shingo upande, nami niligundua kuwa hakuwa ameridhia hali yangu kutoka moyoni mwake. Mchana niliondoka na kwenda nyumbani kwetu wanakoishi mama na familia yote ninayoilea. Sikutaka kabisa kumweleza mama yangu yaliyonikuta kwa sababu yeye alikuwa ni mgonjwa, hivyo sikutaka habari ya kutokuwa na biashara tena imuongezee maumivu ya kumletea kifo.  Nilipanga kubaki na siri hii peke yangu. Nilichokuwa napanga ni kumwambia Rumia tu na si ndugu yangu yeyote yule.

Siku ya pili yake nilirudi jiji Port Villa na kununua mahitaji mengi ya nyumbani nilitumia kiasi kikubwa cha pesa cha shilingi 200.  Nyumbani niliwaletea mahitaji mengi nilifanya hivyo ili yatumike kwa muda mrefu hadi wakati wa kile kipindi cha mateso kitakapofika.

SASA ENDELEA…

Nilihakikisha nanunua mahitaji hayo kwa kukadiria muda ambao nitakuwa sina biashara na wakati wa kutafuta kazi nyingine ya kufanya ili kuninusuru mimi na familia yangu.

Nilinunua unga, mchele, mafuta sukari, sabuni na mahitaji mengine yanayohitajika wakati wowote. Nilinunua vitu hivyo kama vile nilikuwa nafungua duka, mama na ndugu zangu wote walinishangaa kwa sababu sikuwahi kufanya hivyo toka nilipoanza kutegemewa. Waliponiuliza kwanini nafanya hivyo niliwajibu kuwa maisha yanabadilika ni muhimu kuhifadhi mahitaji kabla shida hazijaja.

Hata nyumbani kwangu Rumia alishangaa kuona nanunua mahitaji mengi tofauti na siku zote, aliponiuliza sababu ya kufanya hivyo  nilimwambia kuwa nitamueleza jioni kila kitu. Nilishakuwa nimepanga kumwambia Rumia juu ya kilichotakea Port Villa kwenye biashara yangu sokoni.

Sikuona haja tena ya kuficha kwa siku ya nne, kwani hilo ndilo lililokuwa suala la kupasa kuimarisha ndoa yetu au kubomoa. Niliamini kuwa kumweleza Rumia ukweli ndio kutanionyesha rangi yake halisi, nitajua kuwa ananipenda kutoka moyoni au yuko tu kwa ajili ya uwezo wangu wa kuyamudu maisha.

Hata hivyo, siku zote nilikuwa nikiamini Rumia aliachana na Franco Mazimbe kwa sababu kijana huyo wa Port Villa alikuwa amempata mwanamke mwingine. Niliavaa roho ya ujasiri nikijisemea kuwa kama Rumia ni wangu ni wangu tu na kama si wangu ni si wangu tu. Nilipanga kumweleza usiku nikiwa naye kitandani.

Nilinunua mahitaji mengi na kubakiza kiasi cha shilingi 5,000 pesa iliyokuwa nyingi sana kulingana na maisha halisi. Pesa hiyo ilikuwa imechanganywa na pesa niliyokuwa nayo akiba na ile niliyouza kwa mara ya mwisho kabla sijafukuzwa katika soko la jijini Port Villa.

Niliamini pesa hiyo ndio iliyobeba maisha yangu kwa sababu ilikuwa ni nyingi ambayo ingeniwezesha kutafuta kazi au kuanzisha biashara nyingine tofauti na ile ya matunda na mbogamboga.  Nilikuwa nimeanza kupanga nini cha kufanya, maana biashara yoyote ilifanyika jiji Port Villa au kwingineko kunakokaliwa na kabila la Wahi ambao ndio walioshikilia uchumi wan chi. Huku kwetu Adorra na Kataga hakukuwa na biashara ya kunua wala kuuza kwa sababu watu walikuwa mafukara kiasi cha kushindwa kumiliki shilingi 500.

**********

Usiku wa saa tatu tukiwa tumepumzika chumbani, nilijiweka sawa kwa ajili ya kumweleza mke wangu kila kitu lakini pamoja na ujasiri huo niliojivika, bado nilikuwa nikitetemeka sana, maana niliogopa kumuudhi kwa sababu mimi kwake nilikuwa kichaa wa mapenzi. Akiwa amenilalila juu ya kifua changu, nilihema mara moja na kumwambia.

“Sitapeleka tena mazao Port Villa.”

Alinitazama usoni na kukunja ndita mbili akibaki na mshangao.

“Unamaana gani?” aliniuliza.

“Naaminisha kuwa sina tena biashara kule.”

“Kwanini?”

Nini kitaendelea? Usikose Alhamisi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -