Sunday, October 25, 2020

TAJIRI WA MASIKINI – 5

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

Na Eman Fisima, +255 654 076 265


 

Ilipoishia

Maana ni kweli sura yangu ilikuwa imejawa na huzuni na mashaka makubwa kutokana na kukutana na mpenzi wake wa zamani aliyeniambia maneno yenye ukweli fulani. Nilishindwa kumjibu, alifunikia samaki kwenye sufuria akiiacha inachemka na kuja pale nilipokaa. Alikaa juu ya mkono wa kochi, kochi nililokalia mimi akanishika shavu na kuniuliza tena.

 “Uso wako umechoka si kwa uchovu wa kazi hakika kuna jambo linakusumbua mume wangu, niambie  nini tofauti?”

Niliinua uso wangu nikamtazama sana kisha nikamuuliza.

“Rumia mke wangu hivi unanipenda kweli?”

Alishuka kwenye mkono wa kochi na kunikalia juu ya mapaja yangu khanga yake ikiwa wazi sehemu ya paja lake moja, hali iliyoutesa mwili wangu kihisia. Kwa macho malegevu alinijibu.

“Nakupenda sana Vanuell tena sana.”

“Una hakika hutakuja kuniacha?” nilimuuliza.

“Mimi ni wako Vanuell, tayari sisi ni wanandoa tulioapa mbele ya mashahidi na mbele ya Muumba kwa nini nikuache, usiwe na mawazo hayo mume wangu nakupenda sana.”

Nilimuuliza maswali hayo kwa sababu nilikuwa kwenye ulingo wa kupambanisha maneno ya yule mwanaume wake wa mwanzo na ya kwangu mimi mume wake. Ili nijaribu kupata angalau jibu la tofauti na lile la yule kijana tajiri wa Port Villa.

“Naskukuru mke wangu kwa kunipenda ila ninahofu kidogo,” niliongea kwa wasiwasi.

“Hofu ya nini tena Vanuell wangu?”

“Siku ambayo itatokea mambo yangu yote yakaharibika biashara yangu ikapotea je, utanipenda na utakubali tuendelee kuishi pamoja hapa ndani?”

Aliposikia swali hilo alihema kidogo akaitazama mboga iliyokuwa ikichemka jikoni, kisha akanirudia na kunijibu kwa tabasamu.

Ilipoishia

Aliposikia swali hilo alihema kidogo akaitazama mboga iliyokuwa ikichemka jikoni, kisha akanirudia na kunijibu kwa tabasamu.

“Kwa sasa na hata baadaye pesa na mali si kitu mbele ya ndoa yetu Vanuell, siwezi kukuacha kisa vitu hivyo.”

Maneno hayo yaliingia moyoni mwangu moja kwa moja na kunisahaulisha kidogo maneno ya yule kijana wa Port Villa, maana Rumia aliyaongea kwa hisia na tabasamu pana huku macho yake nayo yakisema kwa ulegevu mzuri.

Alinishika tena shavu la kulia, akanisogele na kunibusu kisha akasema maneno mengine mapya yaliyo mazuri sana.

“Nimekuchagua wewe uwe wangu sikujali kama watu wa Port Villa wamekuzidi kipato, mimi nimeamua kutulia kwa sasa ili niishi maisha ya ndoa, ndio maana nilimuacha yule mwanaume.”

Nilitabasamu nikamtazama kipenzi mke wangu na kusema.

“Asante Rumia wangu maneno yako yamenitoa katika wasiwasi.”

Baadaye alikwenda kuipua mboga kisha akatenga sufuria ya wali na kunijia tena pale kwenye kochi, alinitazama usoni na kuniuliza.

“Kwanini umeniuliza hayo yote mume wangu, kuna tofauti umeiona?”

Sikutaka kabisa kumueleza kuwa nilikuwa nimekutana na yule mwanaume pindi nilipokuwa narudi shambani, nilibaki na siri hiyo mimi mwenyewe.

“Hapana Rumia ni wasiwasi tu niliokuwa nao maana nyinyi wanawake mara nyingi huwa mnabadilika.”

“Usijali mpenzi wala usiwe na shaka nami.”

Alinihakikishia yote na kunifariji, baadaye giza likiwa limekwishakuingia tulikaa mezani na kupata chakula cha jioni. Maisha yangu ya ndoa niliyapenda sana hakika yalinifanya nisahau shida za umasiki na mateso tuliyonayo sisi Wapache watu wa Adorra na Katanga.

Kesho yake niliamka asubuhi kama kawaida yangu ili niwahi shambani kwangu, kabla sijaondoka tulipata kifungua kinywa mimi na mke wangu, baadaye nilimuaga na kuondoka nyumbani. Moja kwa moja nilipitia kwa familia yangu na watu wengine niliokuwa nawatunza, nilipofika huko nilitoa matumizi madogo madogo ya nyumbani kwa pesa ya shilingi nane. Pia Niliwapatia wadogo zangu Satia na Lukia ada ya shule shilingi 20.

Satia na Lukia waliokuwa mapacha walikuwa wakisoma darasa la saba katika Shule ya Msingi Dhifa wakitarajia kuingia darasa la nane.

Baada ya hapo nilielekea shambani kwangu eneo la Kangamuwa, eneo lililokuwa pembezoni kabisa mwa Kitongoji cha Adorra karibu na Katanga likiwa kilomita chache kutokea Mto Vuma.

Wakazi wengi wa Adorra na Katanga waliutumia mto huo kulima mazao ya chakula, lakini ugumu ulikuwa namna ya kupata soko. Haikuwezekana sisi wenyewe kuuzia mazao tuliyolima kwa sababu hatukuwa na pesa, soko la mazao yetu lilitegemea wanunuzi kutoka mji mkuu yaani jijini Port Villa na kwingineko kunakokaliwa na maadui zetu wa ubaguzi yaani Wahai, ambao siku zote walikuwa na msemo wa jeuri, msemo usemao kuwa maisha bila wao hatuyawezi.

Kauli hiyo ilikuwa na ukweli kwa sababu serikali ilikuwa yao na wao ndio walikuwa wameushikilia uchumi wa nchi.

Ni mimi pekee niliyepata bahati ya mtende ya kuwa na rafiki mwerevu aliyekuwa tofauti na Wahai wenzake, kijana Rahimu aliyekuwa akinisaidia kuweka mazao yangu katika sehemu yake katika soko kuu jijjini Port Villa.

********

Kesho yake mida ya saa 11:30 jioni jua likiwa linaelekea kuzama, nikiwa narudi nyumbani kwangu, kama kawaida nilipita mbele ya nyumba ya shangazi yake na Rumia. Nilimkuta yule kijana mwanaume wake na Rumia kabla sijamuoa akiwa ameegama kwenye pikipiki yake, yalikuwa ni mapatano yetu ya kuonana siku ile kama alivyohitaji kujua mahali alipo Rumia na kujua kama ni kweli alikuwa amekwishakuolewa.

Siku hiyo nilipanga kumwambia ukweli ambao juzi nilikua nimeuficha, ukweli wa juu ya kuwa mimi ndiye mume wa Rumia. Sikuwa na ule woga wa juzi tena kwa sababu tayari mke wangu alishakuwa amenihakikishia kuwa mimi ni wake na hatoniacha kamwe. Hivyo nilikuwa na jeuri kidogo ya kumweleza kila kitu.

Nilimsogelea na kuweka mzigo wangu chini niliotoka nao shambani na kisha nikamsalimia.

“Habari yako.”

Alinitazama kwa ile dharau yake ya juzi kisha akanijibu vile apendavyo.

“Si njema sana za shambani kwako?”

“Nzuri tu,” nilimjibu kwa tabasamu.

Kama kawaida yake alichomoa sigara yake aina ya Maruboro na kuiwasha mbele yangu pasipo kujua kuwa mimi nilikuwa sipatani kabisa na moshi wa sigara, alivuta mara moja na kusema.

“Nasubiri jibu kutoka kwako kama jana tulivyokubaliana umefanikiwa kumpata Rumia?”

Nilicheka kidogo kiasi cha kumshangaza kisha nikamwambia neno lililomfanya anitolee macho.

“Mimi ndiye mume wa Rumia.”

Alibaki ameiweka sigara yake mdomoni asiamini kile nikisemacho, baadaye aliitoa kisha akaniuliza.

“Unanitania?”

“Mimi na wewe tulianza utani lini na tokea karne gani makabila yetu yakataniana?” nilimuuliza.

“Nashangaa wewe kuanzisha masihara na mimi wakati ni watu tusioendana kwa kila kitu,” aliongea huku akiitupa sigara yake chini.

“Wewe si ulikuwa unataka kumjua mume wa Rumia? Mimi ndiye, mimi hapa mbele yako.”

Alinicheka kwa mara nyingine kisha akasema:

“Huna hadhi ya kumuoa Rumia na kama ni kweli basi jua Rumia kakuongopea.”

“Sikiliza kaka hayo mengine nadhani ni kupoteza muda, kama ni kujua tayari umekwisha kujua mi naona niache niende.”

“Usiwe jeuri hebu nisikilize kijana. Kama wewe ndiye mume wake jua kabisa Rumia ni wangu mimi. Tambua umepoteza pesa zako kuandaa harusi na mpenzi wangu.”

“Huu ni mwezi wa pili tokea nimuoe Rumia, wewe ulikuwa wapi siku zote na imekuwaje akubali kuolewa na mimi ihali kuwa wewe upo tena mtu mwenye pesa zako?”

“Lakini sitoamini hadi nikutane na Rumia mwenyewe, aniambie huu ukweli batili, maana bado siamini kabisa. Hebu jitazame wewe kisha nitazame na mimi yaani ni dhahiri kabisa hatuendani. Sikiliza hata hivyo nadhani kama Rumia alikubali kuolewa na wewe ni kwa sababu amekuona wewe ni taofuti na vijana wengi katika vitongoji hivi vya umasikini, amekuona  kidooogo unakauwezo, bila hivyo sidhani kama angekubali.”

Nilimsogelea kidogo na kumuuliza.

“Kwa hiyo unaamini kama mimi ndiye au  huamini kabisa kama Rumia kaolewa na Mpache kutoka ardhi masikini ya Andorra?”

Alibaki kunitazama akionyesha mtu mwenye kuikarabisha hasira fulani.

Nini kitaendelea? Usikose kesho

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -