Tuesday, October 20, 2020

TAKUKURU MSICHEZE MBALI MZUNGUKO WA PILI VPL

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA HASSAN DAUDI

MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) unatarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho. Burudani imerejea tena.

Mara nyingi, ni katika mzunguko wa pili ndipo kumekuwa na ushindani mkali, ni tofauti na duru la kwanza.

Binafsi natarajia kuona vita tatu katika mzunguko wa pili. Moja ni ile itakayozihusisha timu zitakazokuwa zikifukuzia ubingwa.

Lakini pia, kutakuwa na vita kali ya timu zitakazokuwa zikihangaikia nafasi ya pili ambayo itawapa tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwa upande mwingine, kutakuwa na mtifuano mkali kati ya timu zitakazokuwa kwenye hatari ya kushuka daraja, kila moja ikipambana kujinasua kwenye janga hilo.

Kwa hali hiyo, mzunguko wa pili utakuwa na upinzani mkali kuanzia kwa timu vigogo hadi zile zinazoaminika kuwa ndogo.

Mara nyingi upinzani huo wa duru la pili huibua vitendo vya rushwa, yaani matokeo ya soka huamuliwa nje ya uwanja.

Kwa maana nyingine, mara nyingi fedha huwa na nguvu kubwa kuamua matokeo ya mechi za mzunguko wa pili.

Imekuwa ni kawaida kusikia vitendo vya kununua mechi na kupanga matokeo kila duru la pili la VPL linapoanza.

Hapo, timu zisizojiweza kiuchumi ndio zinapogeuzwa soko la matokeo.

Kutokana na ukata wa kifedha unaozikabili, wachezaji wake wamekuwa wakicheza chini ya kiwango kwa makubaliano ya kupewa kiasi cha fedha na mabosi wa timu nyingine.

Tegemea kusikia viongozi wa timu ndogo wakilia kupitia vyombo vya habari kuwa walichezewa mchezo mchafu na wenzao wa timu vigogo.

Hata hivyo, huenda tatizo hilo likapungua kwa kiasi kikubwa kama si kutokomezwa kabisa msimu huu, kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) itakuwa macho kuanzia kesho.

Naamini taasisi hiyo ina uwezo mkubwa wa kufuatilia kwa karibu kila hatua ya mzunguko wa pili ili kubaini na kuibua vitendo vya rushwa vinavyoweza kujitokeza.

Mbali na kufichua uhalifu huo wa mchezo wa soka, Takukuru inatakiwa kusimamia na kuhakikisha wanaokamatwa wanaadhibiwa vikali.

Kwa upande mwingine, ingependeza kuona mkono wa Takukuru ukiwafikia waamuzi watakaokuwa wawezeshaji wa vitendo vya rushwa katika michezo ya duru la pili.

Imetokea mara nyingi kusikia na hata kuona marefa wakipewa kiasi fulani cha fedha ili kuibeba timu fulani. Takukuru amkeni mzunguko wa pili kukomesha tabia hii chafu.

Natamani kuiona taasisi hiyo ikiongeza umakini zaidi na kutoa macho kwa kila hatua ya mzunguko wa pili ambao ndiyo hitimisho la VPL kwa msimu huu wa 2016-17.

Nasisitiza kuwa, ile tabia ya kesi za rushwa kupotea kusikojulikana isipewe nafasi katika mzunguko wa pili.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -