Tuesday, October 27, 2020

Takwimu hizi zitampa Mesi Ballon d’Or

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MADRID, Hispania

KWA takribani miaka 10 iliyopita, staa Lionel Messi na mpinzani wake Cristiano Ronaldo, wamekuwa watawala wa ulimwengu wa soka.

Kwa lugha nyepesi na ya kueleweka, unapozungumzia mchezo wa soka, si rahisi sana kuyaweka kando majina ya wakali hao wa Ligi Kuu nchini Hispania ‘La Liga’.

Baada ya kutolewa kwa orodha ya wachezaji 30 wanaowania tuzo ya Ballon d’Or na ile ya Mchezaji Bora wa Shirikisho la Kimataifa (Fifa), wengi wanaamini ni Messi au Ronaldo wenye nafasi kubwa ya kutajwa washindi.

Huku Messi wa Barcelona akisaka Ballon d’Or yake ya sita, Ronaldo atakuwa akitamani kuiweka mkononi kwa mara ya nne.

Hata hivyo, wapo wanaoamini kuwa Messi amezidiwa na Ronaldo hivyo ni ngumu kwa Muargentina huyo kunyakua tuzo hiyo mwaka huu.

Wakati Ronaldo akishinda taji la michuano ya Euro 2016 akiwa na timu yake ya Taifa ya Ureno, Messi aliifikisha Argentina katika hatua ya fainali ya michuano ya Copa America.

Kwa tathmini ya haraka, ni wazi Ronaldo alikuwa na mafanikio makubwa kwenye ngazi ya timu ya taifa.

Lakini wachambuzi wa soka wameibuka na sababu saba ambazo zinaweza kumfanya Messi kuibuka kidedea mbele ya Ronaldo.

Messi ameanza vizuri msimu huu na mpaka sasa nyota huyo ameshapachika mabao 16 katika mechi 14 alizocheza.

Kwa upande wake, Ronaldo ameonekana kuanza taratibu ambapo ameshapachika mabao saba pekee licha ya kushuka dimbani mara 12.

Wakati Messi akiwa na wastani wa bao moja katika kila mchezo anapoingia uwanjani, hasimu wake Ronaldo anayetamba na Real Madrid ana wastani wa 0.58.

Kiwango alichokionesha Messi katika mchezo wa La Liga dhidi ya Sevilla kilikuwa cha ubora wa juu katika maisha yake ya soka.

Ikumbukwe kuwa Barcelona walikwenda ugenini wakiwa na machungu ya kipigo katika mchezo dhidi ya Manchester City.

Katika mchezo huo wa hatua ya makundi uliochezwa jijini Manchester kwenye Uwanja wa Etihad, Barca walichezea kichapo cha mabao 3-1.

Wakiwa ugenini dhidi ya Sevilla, Barca walionekana kukamatwa katika kila idara, wenyeji walikuwa wamejipanga vilivyo kuhakikisha wakali hao hawaondoki na pointi zote tatu.

Barca walikuwa wa kwanza kukubali nyavu zao kutikiswa lakini ni Messi ndiye aliyesawazisha bao hilo zikiwa zimebaki dakika chache kabla ya timu hizo kwenda mapumziko.

Mbali na hilo, jina la Messi lilijitokeza tena kwenye orodha ya wafungaji na kuiwezesha Barca kuzoa pointi zote tatu katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Ramon Sanchez Pizjuan.

Ukiachana na takwimu za msimu huu, kwa kipindi chote alichokaa Barca, Messi ameshinda kombe moja katika kila msimu huu.

Messi alianza kuichezea Barca mwaka 2004 na ni misimu miwili pekee ambayo imepita akiwa mikono mitupu. Messi alikosa ubingwa katika msimu wa 2006-07 na 2013-14.

Ingawa mwaka 2008 Barcelona hawakuchukua taji lolote, Messi alikuwa sehemu ya kikosi cha Argentina kilichoshinda medali ya dhahabu katika michjuano ya Olimpiki.

Kwa kipinjdi chote alichokaa Catalunya, Messi ameiwezesha Barca kushinda mataji 25.

Alipopachika bao katika mchezo wa nusu fainali ya Copa America dhidi ya Marekani, Messi alivunja rekodi ya upachikaji mabao kwenye timu hiyo.

Ni kweli Ronaldo alikuwa sehemu ya kikosi cha Ureno klilichotwaa Euro 2016, lakini ni kweli alifanya kazi kubwa kwenye mashindano hayo?

Staa huyo alifunga mabao matatu pekee katika michuano hiyo iliyofanyika nchini Ufaransa, mawili aliyafunga katika mchezo dhidi Hungary na moja alipokutana na Wales.

Latika mchezo wa fainali dhidi ya wenyeji Ufaransa, mkali huyo alitoka nje katika dakika ya 25 baada ya kuumia kutokana na rafu ya kiungo Dimitri Payet.

Messi alipachika mabao matano akiwa na Argentina katika michuano ya Copa America uliyofanyika Marekani.

Kwa upande wa pasi za mabao, Messi anamfunika vibaya Ronaldo ambaye ni hasimu wake mkubwa kwenye ulimwengu wa soka.

Tangu kuanza kwa msimu huu, pasi za mwisho za Messi zimesaidia kupatikana kwa mabao saba huku asisti za Ronaldo zikizaa mabao matano pekee.

Lakini pia, Messi ndiye mchezaji pekee barani Ulaya ambaye ameweza kugusika kwenye idadi kubwa ya mabao akifanya hivyo mara 23.

Kwa kipindi chote alichokutana na Madrid, Messi amewafunga matajiri hao wa jijini Madrid mara 21 huku akitoa asisti 13.

Wakati Muargentina huyo akifanya hivyo, Ronaldo amewafunga Barca mabao 16 huku pasi zake zikizaa mabao mawili pekee katika michezo yote aliyokutana na Wacatalunya hao.

Kwa upande mwingine, wapo wanaoamini kuwa Messi amekuwa bora kutokana na uimara wa kikosi cha Barca lakini si kweli. Nyota huyo amekuwa akithibitisha maklali yake hata anapokuwa na kikosi cha Argentina.

Argentina inapokuwa uwanjani, ni rahisi kuuona umuhimu wa Messi kuliko Ronaldo anapokuwa na Ureno na imekuwa hivyo kwa miaka kadhaa sasa.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -