Sunday, January 17, 2021

Tamasha la Bagamoyo kuanza leo

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA STELLA KANYARI, TUDARCO

TAMASHA la kimataifa la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo, linaanza leo mjini Bagamoyo huku Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, akitarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa tamasha hilo.

Tamasha hilo kongwe la sanaa za maonyesho katika ukanda wa Afrika Mashariki hufanyika kila mwaka na litafanyika kwenye viwanja vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) likiwa limeratibiwa na taasisi hiyo chini ya Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo na mwaka huu tamasha hilo litafanyika kwa mara ya 35.

Ni tamasha ambalo hujumuisha sanaa zote za jukwaani ikiwemo ngoma za asili, sarakasi, maigizo, mazingaombwe na muziki  lakini pia huwa na maonyesho maalumu ya sanaa za ufundi na warsha mbalimbali kuhusu masuala ya sanaa.

Tamasha hilo lilianza mwaka 1982 ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kuanza kwa kilichokuwa Chuo cha Sanaa Bagamoyo (sasa TaSUBa) na lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya mitihani ya vitendo kwa wanafunzi.

Mwaka huu tamasha hilo litashirikisha vikundi vipatavyo 65, kati ya hivyo vikiwemo vya ndani na vingine kutoka nje ya Tanzania ambapo nchi za Kenya, Norway, Ujerumani, Argentina na Ivory Coast zimetuma vikundi vyao kwa ajili ya kushiriki tamasha hilo mwaka huu.

Lengo kuu la Tamasha la Bagamoyo kwa sasa ni kutoa fursa kwa wasanii wa ndani hasa wanafunzi wa TASUBa kubadilishana uzoefu na kujifunza kutoka kwa wasanii wengine lakini pia lengo lingine ni kuonyesha ufahari wa sanaa za asili za Tanzania kwa kuwa hilo ndilo tamasha pekee kubwa la sanaa za maonyesho linalotoa nafasi ya sanaa za asili kufanyika hapa nchini.

Mbali na kuvikutanisha vikundi mbalimbali vya sanaa vya ndani na nje ya nchi kwa nia ya kubadilishana ujuzi juu ya masuala ya sanaa, lakini tamasha hili lina maana kubwa sana kwa TaSUBa ambapo hulitumia kama sehemu ya mafunzo kwa wanafunzi, jukwaa la tamasha kutumiwa na wanafunzi kufanya mazoezi kwa vitendo, wanafunzi hushindana kwa kuonyesha kazi zao za sanaa na walimu huchukua alama mlimbiko ambazo huingizwa kwenye rekodi ya mitihani yao.

Kwa wakazi wa Bagamoyo na maeneo jirani tamasha hili pia lina maana kubwa sana kwani  limekuwa sehemu ya ratiba yao ya mwaka, limekuwa pia ni sehemu nzuri ya kukuza na kutangaza utalii wa urithi wa utamaduni mji wa Bagamoyo, hivyo limekuwa na mchango mkubwa pia katika sekta ya ukuaji wa utalii hapa nchini.

Ratiba ya ufunguzi itaambatana na chakula maalumu cha Kikorea kilichoandaliwa na ubalozi wa Korea nchini Tanzania kabla ya ratiba kamili ya ufunguzi kuanza kwa hotuba na maonyesho ya jukwaani.

Zaidi ya watu 1,500 uhudhuria tamasha la Bagamoyo kuanzia maonyesho ya sanaa za ufundi ambazo huanza asubuhi na maonyesho ya jukwaani ya mchana na usiku. Kaulimbiu ya tamasha la mwaka huu ni sanaa na utamaduni kwa maendeleo ya vijana.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -