Wednesday, October 21, 2020

TAMBWE AIPIGIA HESABU KALI MWADUI

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA ESTHER GEORGE

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amissi Tambwe, amepiga hesabu kali ya ushindi dhidi ya Mwadui katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA jana, Tambwe alisema atahakikisha wanaondoka na pointi tatu ili waweze kuwaengua kileleni watani wao wa jadi Simba.

Tambwe ambaye amefunga mabao tisa, alisema wanahitaji ushindi wa hali na mali ambao utawawezesha kutetea ubingwa wao na kuendelea kushiriki michuano ya kimataifa.

Alisema anaamini kwamba mazoezi waliyofanya yatawawezesha kupata matokeo mazuri, licha ya kwamba wapinzani wao nao wanahitaji kupata pointi tatu.

“Kwa mazoezi tuliyoyafanya Mwadui lazima wakae kwani tumedhamiria kuondoka na pointi tatu ambazo ni muhimu kwetu ili tuweze kutetea ubingwa,” alisema Tambwe.

Tambwe alisema pamoja na mchezo huo utakuwa mgumu, lakini watapambana kuhakikisha ushindi unapatikana.

Yanga inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 43 huku Simba wakiwa kileleni kwa pointi 45.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -