Monday, November 23, 2020

TAMBWE AWASHTUA YANGA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MWANDISHI WETU


MSHAMBULIAJI wa Yanga raia wa Burundi, Amisi Tambwe, amewashtua viongozi wa klabu hiyo ambao wanaonekana hawana mpya wa kumwongezea mkataba wa kuendelea kukipiga  katika kikosi hicho.

Tambwe alitemwa na Simba katika msimu wa usajili wa dirisha dogo la 2014 la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kujiunga na Yanga, sasa  amebakisha miezi minne kuitumikia klabu hiyo.

Pamoja na kubakisha muda huo, viongozi wa Yanga hawajaonyesha nia ya kumwongezea mkataba mwingine mshambuliaji huyo aliyetokea klabu ya Vital’ ya Burundi kabla ya kutua Simba na baadaye Jangwani.

Akizungumza na BINGWA jana, Tambwe alisema  mpaka sasa hajafanya mazungumzo na viongozi wake kuhusu kumwongezea mkataba mwingine  ili aweze kuitumikia klabu hiyo.

Tambwe alisema  kwa sasa amebakisha miezi minne kumaliza mkataba  wa kuichezea Yanga na anaweza kufanya mazungumzo na klabu yoyote itakayohitaji huduma yake.

“Bado sijafanya mazungumzo na viongozi wa kamati ya usajili, mkataba wangu unaisha Aprili mwakani,” alisema Tambwe.

Katika hatua nyingine, Tambwe alisema wanaendelea kujipanga  kufanya vizuri zaidi msimu huu kutokana na vitu adimu anavyopewa na kocha mpya wa timu hiyo, Mzambia Goerge Lwandamina, katika mazoezi yanayoendelea kwenye Uwanja wa Gymkhana jijini Dar es Salaam, kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Tambwe amekuwa akipata mbinu mpya ya kucheza soka baada ya kocha Hans van der Pluijm kupewa majukumu ya ukurugenzi ndani ya klabu hiyo.

Mshambuliaji huyo amekuwa mfungaji bora katika misimu miwili tofauti Ligi Kuu Bara, alifunga mabao 19 katika msimu wake wa kwanza akiwa na Simba na msimu uliopita alifunga mabao 21 Yanga.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -