Thursday, October 22, 2020

TAMBWE: HAKUNA WA KUTUZUIA YANGA

Must Read

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

NA ZAINAB IDDY

MSHAMBULIAJI wa Yanga raia wa Burundi, Amis Tambwe,  haoni kama kuna timu inaweza kuwazuia Yanga kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Tanzania msimu huu.

Akizungumza na BINGWA jana, Tambwe alisema mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakuwa mwepesi kwao kutetea taji lao na ana uhakika wa kulitwaa kombe hilo kwa mara nyingine kutokana na ratiba ya mzunguko wa pili kuonyesha mechi nyingi watacheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Tambwe alisema mzunguko wa kwanza mechi nyingi walicheza ugenini, hali iliyowafanya washindwe kupumzika kutokana na safari za kwenda mikoani kucheza mechi zao.

“Ukiangalia mzunguko wa kwanza, mechi nyingi tulicheza nje ya Dar es Salaam, lakini sasa naona mteremko katika harakati za kutetea taji letu.

“Ratiba ni rafiki kwetu, kwani mechi nyingi tutakuwa Dar es Salaam, hivyo suala la uchovu wa kusafiri litapungua, na hii inatuongezea nguvu za kuhakikisha wa kutetea taji letu,” alisema Tambwe.

Tambwe ameifungia Yanga mabao saba sawa na Simon Msuva wa timu hiyo na Rashid Mandawa wa Mtibwa Sugar katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na Staa Wako, safu inayokupa nafasi...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -