Friday, October 23, 2020

Tambwe: Nitafanya kazi na Lwandamina

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA HUSSEIN OMAR

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amis Tambwe, amesema atahakikisha anafanya kazi itakayomridhisha kocha mpya wa timu hiyo raia wa Zambia, George Lwandamina.

Lwandamina anatarajia kutua Yanga baada ya Mholanzi, Hans van der Pluijm, kuandika barua ya kujiuzulu kwa hofu ya kutimuliwa baada ya kupata tetesi za ujio wa Mzambia huyo.

Akizungumza na BINGWA jana, Tambwe alisema Pluijm anaondoka baada ya uongozi wa klabu hiyo  kumpa mkataba wa miaka miwili Lwandamina, aliyetokea Klabu ya Zesco ya Zambia.

Tambwe alisema maisha ya wachezaji wa soka na makocha ni mafupi kwenye timu, kwani wakati wowote wanakuwa wa kutimuliwa, lakini Pluijm alikata tamaa mapema kutokana na uamuzi wake wa kuachia ngazi.

Tambwe alisema katika maisha ya soka lolote linaweza kujitokeza,  kutimuliwa mchezaji au kocha na hii inatokana na mipango ya Mwenyezi Mungu.

“Hili suala lililotokea ni la kawaida tu, hakuna haja ya kushtushwa hata kidogo, inauma kutokana limetokea ghafla, ila kocha asikate tamaa, ndiyo maisha ya mpira,” alisema Tambwe.

Katika hatua nyingine, Tambwe alisema hatishwi na ujio wa Lwandamina katika kikosi hicho,  badala yake ataifanya kazi yake kadri iwezekanavyo na kuifungia mabao timu yake.

“Mimi sina tatizo, mwache aje tu, nitafanya kazi yangu kama ilivyokuwa kwa Pluijm, sitishiki na ujio wake, hata akimleta nani sisi tutafanya kazi yetu,” alisema Tambwe.

Lwandamina anatarajia kuanza kuifundisha timu hiyo wakati wowote kuanzia sasa kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa mwakani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -