Monday, January 18, 2021

TANZANIA KUUNGANA NA BRAZIL KUOMBOLEZA VIFO VYA WACHEZAJI

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA MARY PETER ,TSJ

SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa(FIFA),limelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ,kama wadau wake kuhakikisha wachezaji wanafunga vitambaa vyeusi kwenye mechi mbali mbali linazozisimamia kama ishara  ya kuomboleza vifo vya wachezaji wa timu ya Chapecoense ya Brazil waliofariki katika ajali ya ndege               .

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, alisema jana kuwa FIFA imewataka  nchi wanachama wake kuhakikisha wachezaji wanafunga vitambaa vyeusi kama ishara ya  kuomboleza msiba huo uliolikumba taifa la Brazil.

“FIFA wametutaarifu sisi kama wanachama wao kuwaelekeza a wechezaji wetu kujumuika nao katika maombolezo kwa kufunga vitambaa vyeusi  watakapokuwa wakati wa mechi ,na kwakufanya hivyo tutakuwa pamoja na nchi zingine duniani katika maombolezo hayo”alisema Lucas.

Msafara wa timu ya Chapecoense ulipata ajali ndege Novemba  28  mwezi uliopita ukiwa unaelekea mjini Medeline nchini Colombia  kwaajili ya mechi ya michuano ya Copa Sudaamericana,ambapo watu 76  walifariki.

Mechi hiyo ya mkondo wa kwanza ilipangwa kuchezwa katika Uwanja wa Atanasio Girardot kabla ya timu hizo kurudiana nchini Brazil.

Kutokana na ajali hiyo mechi hiyo haikufanikiwa kufanyika.

Tukio hilo la kusikitisha limeikumbusha dunia ajali nyingine zilizowahi kutokea miaka ya nyuma zikizikumba misafara ya timu za soka ambazo ni timu ya  Taifa ya Zambia ‘Cipolopolo’,timu ya Manchester United  ya England na timu ya Torino ya Italia.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -