Thursday, October 22, 2020

TANZANIA YA VIWANDA SAWA, LAKINI VIPI MEDANI YA MUZIKI?

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA SELEMANI ALLY, TSJ

KUMEKUWA na madai kuwa muziki wa sasa si lolote na ule wa zamani ukielezwa ulikuwa na mvuto wa kipekee kutokana na tungo, uimbaji pamoja na maudhui yake.

Pamoja na madai hayo, lakini hakuna mwanamuziki au msanii yeyote wa zamani aliyeweza kutikisa nje ya nchi zaidi ya kuishia kwa majirani zetu Wakenya.

Hali ni tofauti na sasa ambapo japo wasanii wa kizazi hiki wamekuwa wakibezwa, lakini wamefanikiwa kufanya mambo makubwa nje ya mipaka ya Tanzania na kuwafunika wale wa zamani.

Hapa Tanzania msanii wa kizazi kipya, Nasib Abdul ‘Diamond’, ameweza kufanya vizuri na kupata mafanikio makubwa.

Ingawa hatuangalii kipato pekee kwenye muziki, lakini ukweli ni kwamba wasanii wengi huimba na lengo kubwa likiwa ni kujipatia kipato.

Muziki wa Tanzania kama ungepewa heshima, naamini ni sehemu moja kubwa na ya kipekee katika kulitangaza taifa na rasilimali zilizopo nchini mwetu.

Hakuna namna nyingine ya kuupa heshima muziki wetu kama Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) na wasimamizi wa haki miliki (Cosota) hawatahakikisha kazi za msanii zinalindwa ili kuleta masilahi kwa msanii husika.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Cosota walikuja na mbinu ya kutaka vyombo vya habari kulipia code kwa kazi za wasanii wanazozitumia, lakini sijui hizo mbinu zimepotelea wapi.

Takwimu zinaonyesha ni vituo vichache sana vinavyofuata sheria hiyo, je, Cosota hawalioni hilo?

Muziki umekuwa kama kazi kwa vijana wetu kujiajiri wenyewe na kuacha kukaa masikani kujadili mambo yasiyo na msingi, hivyo ni lazima uheshimiwe ili kuleta mafanikio kwa msanii mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Kutokana na juhudi zake binafsi, msanii Ambwene Yesaya ‘AY’, mwaka 2009 aliiwakilisha vema Tanzania kwa kuwa mshiriki pekee kwenye tuzo kubwa Afrika zinazojulikana kama Chanel O Music Awards, zilizofanyika Afrika Kusini.

Ingawa wapo Watanzania ambao waliwahi kuwa washiriki katika tuzo mbalimbali duniani, lakini hakikuwa kama kipindi kile cha AY.
Baada ya AY kuwa mshiriki wa tuzo hizo kubwa barani Afrika, alimpatia fursa msanii mwenzake kutoka Tanzania, Diamond, nafasi ya kufanya nyimbo kwa kumkutanisha na msanii maarufu kutoka Nigeria, Davido, ambaye kwa kipindi hicho alikuwa akitamba na kibao cha Skelewu.
Diamond alipopata nafasi hiyo aliamua kurudia wimbo wake uliojulikana kwa jina la ‘My Number One’ alioufanyia remix pamoja na mkali huyo kutoka Nigeria.

Tukiacha ushabiki, baada ya wimbo huo kutoka ulifanya vizuri ndani na nje ya nchi kuliko nyimbo zake zote alizowahi kufanya msanii Diamond.

Hii ilikuwa ni sababu ya yeye kuchaguliwa kuwania tuzo kubwa kwa mara ya kwanza nchini Nigeria, tuzo za MTv na kufanya shoo katika tuzo hizo.

Baadaye Diamond alizidi kushiriki katika kuwania tuzo hizo kila mwaka na nyingine za kimataifa ambapo amefanikiwa kuchukua baadhi yake na kuwashinda wapinzani wake.

Kwa sasa ukizungumzia tuzo zozote Afrika huwezi kuacha kuizungumzia Tanzania, kwani ni moja kati ya nchi zinazotoa washiriki wengi kuwania tuzo mbalimbali barani Afrika, lakini wengi wao ni juhudi binafsi.

Ahsante Ambwene Yesaya na Nasibu Abdul, kwani bila wao siamini kama tungefika hapa tulipofikia kwa sasa.

Na tafiti zinaonyesha kuwa kila kukicha wasanii kutoka Tanzania wanazidi kuongezeka kwenye washiriki wa kugombania tuzo mbalimbali Afrika, akiwamo msanii Ali Kiba, ambaye alishinda tuzo ya Best African Act hivi karibuni.

Diamond alishinda tuzo tatu mfululizo za AFRIMA na kuzileta nyumbani Tanzania mwezi uliopita, Harmonize amenyakua tuzo ya msanii bora anayechipukia barani Afrika.

Mafanikio yao yamewezesha Tanzania kujulikana kimataifa katika tasnia ya muziki, lakini tumeamua tuwe na Tanzania ya viwanda, tunajiuliza vipi medani ya muziki?

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -