Tuesday, November 24, 2020

TASUBA YAJIIMARISHA MAFUNZO YA SAUTI NA VIDEO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, juzi alizindua vifaa vya mafunzo ya uandaaji wa sauti na picha za video vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni ya Bagamoyo (TaSUBa), ambavyo vimenunuliwa kutokana na fedha za maendeleo zilizotolewa na Serikali.

TaSUBa iliomba shilingi milioni 300 kwa ajili ya mradi wa ukarabati wa miundombinu ya taasisi hiyo, ikiwamo kuimarisha studio zake mbili za sauti na video ambazo ni sehemu salama sana ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wanaosoma masomo hayo chuoni hapo.

Kati ya fedha hizo ambazo ziliombwa kwenye Bajeti ya Mwaka 2016/17, hadi sasa Serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni 100 tu ambazo zimefanikisha sehemu tu ya mradi huo ambayo ni kununua vifaa mbalimbali vya kisasa vya studio hizo mbili.

Akizindua na kukabidhi vifaa hivyo, Waziri Mwakyembe, kwanza aliipongeza taasisi hiyo kutokana na kununua vifaa vingi vilivyo bora kwa fedha kidogo waliyoipata lakini pia kwa kutumia fedha hizo katika malengo yaliyokusudiwa.

“Mmenifurahisha sana, nawapongeza sana kwani mmepewa fedha kidogo mmenunua vifaa bora kabisa vya kisasa, maana mimi ni mwanahabari najua vizuri vifaa hivi na kama vingekuwa famba ningewaambia hapa hapa, lakini kwa kweli hivi ni vifaa bora na vya kisasa kabisa, hongereni sana,” alisema Waziri Mwakyembe.

Miongoni mwa viafaa ambayo vimenunuliwa na TaSUBa katika mradi huo ni pamoja na Mixer ya kisasa kwa ajili ya kurekodia muziki, spika za studio za kisasa (studio monitor), kamera mbili za video za kisasa, vidhibiti mwanga (reflectors), vinasa sauti, Microphones, seti ya televisheni pamoja na vifaa vingine ikiwamo viyoyozi kwa ajili ya studio hizo.

Akizungumzia umuhimu wa taasisi hiyo, Waziri Mwakyembe alisema TaSUBa ni taasisi muhimu sana kwa kuwa imebeba roho ya utamaduni wa Taifa, hivyo ni muhimu sana Serikali ikaweka nguvu zaidi katika kuiendeleza taasisi hiyo.

“Kwanza nikiri kwamba nimejifunza mambo mengi sana, nilikuwa nasikia tu kuhusu hiki chuo, sikujua vizuri na nina hakika huko serikalini tuko wengi ambao hatufahamu vizuri juu ya TaSUBa, wabunge wengi, mawaziri wengi pia hawafahamu taasisi hii.

“Nitazungumza na Mheshimiwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ili kuwaleta mawaziri na wabunge pia waje hapa wajionee na wajifunze ili waelewe mnafanya nini kwa faida ya Taifa letu,” alisema Waziri Mwakyembe.

 

Pamoja na mambo mengine, Waziri Mwakyembe aliahidi kushughulikia fedha zilizobaki kwa ajili ya taasisi hiyo katika mwaka huu wa fedha zipatikane ili taasisi hiyo ikamilishe mradi wake wa ukarabati, kwani amejionea majengo yalivyochakaa yakihitaji ukarabati wa haraka.

“Nitahakikisha hizi fedha kiasi cha milioni 200 zinaletwa, nimeona jinsi majengo yetu yalivyo, yanahitaji ukarabati kwa kweli na niwahimize kwamba hizi changamoto mlizozitaja hapa kwenye risala zenu, kwangu mimi nazitumia kama fursa ya kujifunza kushughulikia mambo yenu,” alisema.

Pia Waziri Mwakyembe aliahidi kuiunganisha taasisi hiyo na mabalozi wa nchi mbalimbali ili kujenga ushirikiano wa kiutamaduni katika kubadilishana uzoefu na ujuzi kwenye sekta ya sanaa hasa katika nyanja ya mafunzo.

“Naomba tu msiniangushe, lakini pia nitazungumza na watu wa TBC (Shirika la Utangazaji Tanzania) waweze kuwatangaza hata mara moja kwa siku, mnafanya mambo makubwa lakini hamjulikani na hii nawapa kama changamoto, mjitangaze mfahamike,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -