Wednesday, October 28, 2020

TATIZO SI NAFASI YA MWISHO, ANAJUA ALIPOKOSA?

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

HAKUNA binadamu asiyewahi kukosea. Kukosea ni suala ambalo lipo tu! Kila binadamu bila kujali hadhi yake wala umri, hukosea. Japo pia kunakukosea kimakusudi ambapo kwa mtu mwenye kujali na kutambua thamani ya kitu au mtu huwa na uwezo wa kuepuka. Kwa kuwa kuna kukosea na hakuna binadamu mwenye uwezo wa kuishi kimalaika, pia inabidi kila mmoja anayekosea asamehewe na kupewa nafasi nyingine.

Hii nafasi nyingine kimsingi si maana yake inaonesha kuwa umezoea kukosewa au kuwa kosa ulilofanyiwa halikuwa kubwa, hapana. Nafasi hii huwa mahususi kumpa mtu aoneshe ni kwa namna gani kosa alilofanya hakulitarajia na anajutia. Nafasi hii huwa dhihirisho la namna unavyomhitaji mhusika.

Kwa sababu ni wazi kuwa huwezi kumsamehe na kutaka kurudiana na mtu ikiwa humhitaji katika maisha yako. Japo unaweza kumpa nafasi hii na kukatokea akakukosea tena, ila huwa hatutarajii kuwa atakukosea kwa kosa kama hili. Kwa mtu mwenye kutambua thamani yako na maana ya kuwa na wewe anaweza kuwa na uwezekano mkubwa sana wa kukosea kwa sababu yeye ni binadamu ila ni kwa asilimia ndogo sana anaweza kukukosea kwa aina hii ya kosa.

Umeumizwa sana na mpenzi wako? Amekufanyia mambo ambayo hutarajii na kufanya upate maumivu makali sana katika nafsi yako? Japo unaumia ila bado unahisi kumpenda? Japo TATIZO SI NAFASI YA MWISHO, ANAJUA ALIPOKOSA? unamuona kama hafai ila unahisi umuhimu wake katika maisha yako bado mkubwa. Si ndiyo? Ndugu yangu, kukosea kupo. Hakuna binaadamu asiyewahi kukosea.

Hata vitabu vya dini vinasema kuwa ni malaika tu ndiyo hawajawahi kukosea, ila tofauti na hapo karibu viumbe wote wamewahi kukosea ikiwa pamoja na Mitume wengi. Haya matabasamu pamoja na vicheko unavyosikia kila siku nyumbani kwetu haina maana tunaishi kimalaika.

Tunakoseana na pengine huwa tunakoseana sana kuliko ulivyowahi kukosewa. Ila kama binadamu wenye akili na wenye kutambua kuwa kukosea ni moja ya hulka za kibinadamu huwa tunatulia chini, tunakanyana kwa namna inavyofaa na maisha yanaendelea. Na kwa kuwa kila mmoja anamjali na kumuheshimu mwenzake, huwa tunasahau yote yaliyotokea na kufungua ukurasa mpya wa mahusiano yetu. Ila kabla hujaamua kusema “nimekusamehe mpenzi wangu”, anajua kama kweli alikukosea? Anafahamu thamani ya chozi na maumivu aliyokusababishia? Japo ni uungwana kumpa mtu nafasi ya pili ila ni ujinga kumpa nafasi ya pili mtu asiyejali, anaona kukosea kwake haikuwa inshu kubwa. Anadhani kuwa kwa kuwa yamepita basi yaachwe yapite. Japo hatupaswi kuishi na kumbukumbu za maumivu yaliyopita ila si rahisi kuzitoa kumbukumbu hizi kama mhusika haoneshi kuwa anajutia na anaumia kwa kile alichosababisha katika maisha yako. Katika mapenzi mkosefu anabidi kuwa mnyenyekevu maradufu. Anabidi kuwa tayari kuwa mpole na ‘mjinga’ kwa dakika zote anazoomba msamaha kwa mhusika.

Hii angalau humfanya mhusika ahisi amani na kuona kuwa mbali na yote ila bado thamani yake kwa mwenzake ipo. Ukiona umekosewa na mkosaji anaomba msamaha kwa ‘kawaida sana’, hapo inabidi ujiulize kama kweli anamaanisha. Kusababishiwa maumivu na bado mhusika kuona kama alichofanya si kitu ujue kuna walakini hapo. Kama kweli anahitaji nafasi ya pili kwa dhati inabidi aoneshe hali hiyo katika matendo na kauli zake.

Inabidi awe tayari kukusikiliza, kukulilia na kukuona mfalme/ malkia katika dakika zote za kukuomba msamaha. Kufanya hivi haimaanishi utumwa. Kufanya hivi haina maana kuwa wewe mkosewaji ni mzuri sana au tajiri sana, hapana. Hii ni tiba katika akili ya mkosewa. Anapaofanyiwa hivi huona kuna hali ya kuonekana wa maana na wa thamani. Hapa hata akisema kuwa nimekusamehe basi msamaha huo hutoka moja kwa moja katika nafsi yake na huwa unamaanisha kauli. Hata kama kuna nafasi ya pili katika makosa ila nafasi hii haimhusu mtu asiyejua ukubwa wa kosa lake na maumivu ya jeraha aliyokusababishia. Tunasamehe ila ni kwa wale wenye kuonesha kwa dhati kuhitaji msamaha na kuona mahali walipokosea. Ahsanteni.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -