Wednesday, October 28, 2020

TAWF WACHAGUE VIONGOZI WAPYA WENYE TIJA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA GLORY MLAY

SHIRIKISHO la Mieleka la Ridhaa (TAWF), linatarajiwa kufanya uchaguzi wa viongozi wake Oktoba 27, mwaka huu, katika Ukumbi wa Msasani Beach Club, jijini Dar es Salaam.

Nafasi mbalimbali zinatarajia kuwaniwa katika uchaguzi huo ambazo ni Rais na Makamu wake, Katibu mkuu na msaidizi wake na Mhasibu mkuu.

Nafasi nyingine inayohitaji kiongozi ni ya Ofisa habari na wajumbe watatu kwa mujibu wa katiba ya shirikisho hilo.

Binafsi nitumie nafasi hii kuwatakia kila la heri TAWF kuelekea uchaguzi wao huo ambao naamini utakuwa huru na wa haki.

Lakini wakati wajumbe watakaopiga kura kuchagua viongozi wa mieleka wakiwa wanajiandaa kwa tukio hilo, ni vema wakafahamu kuwa shirikisho hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinalifanya lionekane kama halipo.

Moja ya changamoto hizo ni viongozi kutokuwa wabunifu, wakishindwa kuendesha mashindano ya kuibua na kuendeleza vipaji vya mchezo wa mieleka.

Matokeo yake, timu nyingi za mieleka zimesheheni wachezaji wale wale wa miaka ya nyuma ambao kimsingi umri umewatupa mkono kiasi cha kushindwa kutoa burudani inayostahili katika mashindano mbalimbali ya mchezo huo.

Mwisho wa siku yote hayo yanafanya shirikisho hilo kuwa la matukio na ukikaribia uchaguzi, ndio kunaendeshwa mashindano lakini baada ya hapo kila kitu kinapotea.

Kwa mazingira kama hayo, binafsi naliona shirikisho hilo kuwa kama la muda mfupi tu.

Shirikisho hilo haliwezi kukidhi matakwa ya wachezaji na wadau wa michezo nchini hasa kwa nyakati hizi ambazo michezo ni zaidi ya burudani, ikitoa ajira inayolipa mno kuliko hata ilivyo kwenye kazi nyinginezo.

Naamini kwamba, shirikisho hilo kikifanya jitihada za dhati kwa kushirikiana na wadau wa michezo nchini, linaweza kufanya mambo makubwa kwa manufaa ya wachezaji, mchezo wenyewe na taifa kwa ujumla.

Na kwa kuwa wiki zijazo shirikisho hilo linatarajia kupata viongozi wapya, nitoe wito kwa watakaochaguliwa kufufua dhana iliyoanza kujengeka miongoni mwa wadau wa mieleka kuwa shirikisho hilo ni la msimu.

Watakaochaguliwa wahakikishe wanajitoa kadiri ya uwezo wao wote kuuendeleza mchezo huo, lakini wakiwashirikisha wadau kwani sote tunafahamu kuwa ‘Umoja ni Nguvu, Utengano ni Udhaifu.’

Kila la heri wapiga kura katika uchaguzi wa mieleka, nikiamini mtachagua viongozi wenye sifa zinazostahili ili kuufikisha mbali mchezo huo, ambao miaka ya nyuma ulikuwa ni maarufu kama lilivyo kwa soka.

Naamini kwamba, shirikisho hilo likifanya jitihada za dhati kwa kushirikiana na wadau wa michezo nchini, linaweza kufanya mambo makubwa kwa manufaa.

Kuzorota kwa mchezo huo kumetokana na kutokuwapo kwa mikakati imara na thabiti ya kuukuza na kuuendeleza mchezo huo, hiyo inatokana na viongozi wengi waliopo TAWF kufanya kazi kimazoea.

Wadau wa michezo hapa nchini wanaona kuna haja ya kubadilisha mfumo uliopo hivi sasa wa uendeshaji wa TAWF kutoka kwenye mfumo wa mazoea wa kukimbizana na kalenda ya matukio na kuruhusu ubunifu zaidi.

Naamini hali hiyo imetokana na mfumo mbovu wa umimi uliotengenezwa na uongozi uliopo madarakani wa kutaka kila kitu akifanye mtu mmoja, jambo ambalo ni adui mkubwa katika maendeleo ya mchezo wowote nchini.

Ni matumaini yangu kwamba TAWF itajiangalia upya hasa katika mwaka ujao na kupokea mawazo mapya ya kiuendeshaji na kutoa nafasi pia kwa wadau wengine kuchangia mawazo yao juu ya kuendesha kwa faida ya mchezo huo na taifa kwa ujumla.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -