Sunday, November 29, 2020

TAYANA WILLIAM: WANAWAKE TUMEWEZA KUITANGAZA GOFU KIMATAIFA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA SHARIFA MMASI

NOVEMBA 11 mwaka jana, kule nchini Uturuki ilifanyika michuano ya wazi ya mchezo wa gofu iliyoshirikisha wachezaji kutoka nchi 61.

Miongoni mwa nchi hizo ni Tanzania iliyowakilishwa na mwanadada, Tayana William, anayeichezea Klabu ya Gymkhana ya Dar es Salaam.

Baadhi ya nchi zilizoshiriki michuano hiyo mbali ya Tanzania ni wenyeji Uturuki, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Afrika Kusini, India na Marekani ambayo ilitwaa ubingwa.

BINGWA limefanya mahojiano na Tayana ili kutaka kufahamu mengi kuhusiana na mchezo wa gofu.

Tayana ambaye alifanya vizuri katika michuano hiyo anasema alifanikiwa kushika nafasi ya tisa na kudai kuwa imemjenga.

“Mashindano yangu ya mwisho kushiriki nje ya nchi ni haya ya Uturuki ambayo yamenifunza mengi yatakayonivusha hapa nilipo na kunipeleka kimataifa.

“Kwanza hii safari ilikuwa na changamoto nyingi sana, napenda kusema kwamba bado viongozi wa mchezo huu wamejisahau katika kutekeleza majukumu yao,” anasema Tayana.

Anasema ushirikiano baina ya wachezaji na viongozi wa juu wa mchezo wa gofu  hauridhishi, anatolea  mfano wakati anajiandaa na safari hiyo, wengi walimkatisha tamaa na hata aliporudi pamoja na kukamata nafasi nzuri bado hawakuonekana kujali.

“Napenda kusema kwamba kama viongozi wa juu wa mchezo huu hawatabadilika basi hatutafika pale tunapopataka, mfano mzuri safari yangu ambayo kama nisingepambana  nisingekwenda kabisa.

“Nilikatishwa tamaa kwa kuonekana sina kiwango cha kwenda kushiriki, lakini namshukuru Mungu nilipokewa vizuri, hali ile ilinifanya nijiamini hadi nikafanikiwa kukamata nafasi ya tisa ukizingatia maandalizi niliyofanya kabla ya safari,” anasema Tayana.

Akizungumzia changamoto anasema kubwa ni michezo hapa nchini kutopewa kipaumbele kama ilivyo kwa mataifa yaliyoendelea.

“Si gofu tu mpaka huko kwenye soka matokeo kila siku ni mabaya, ukichunguza kwa umakini viwango vya wachezaji ni vizuri, tatizo hatuthamini michezo yetu.

“Nafikiri bado viongozi hawajajua kusimamia michezo ipasavyo, endapo watasimama kidete kuendeleza vipaji vilivyopo bila shaka hii nchi itakuwa mbali sana kimichezo,” anasema Tayana.

Tayana anasema, njia nyingine itakayosaidia nchi kupiga hatua kubwa katika michezo kutoa kipaumbele kwa wanawake ambao kwa sasa wanaonekana si kitu.

“Ipo haja ya kubadilisha fikra za watu wenye kuamini kwamba wanawake si kitu katika kuleta maendeleo ya jambo lolote hususani kwenye michezo.

“Wanawake wengi tuna uwezo mkubwa kuliko hata wanaume, ni vema viongozi wakatumia uwezo wetu kuhakikisha wanatusimamia ili tulete mapinduzi makubwa katika soko la michezo hapa nchini,” anasema Tayana.

Tayana anasema tangu anze kucheza gofu mwaka 2010, akiwa kama mbeba mabegi (cady), amejifunza mengi ikiwa ni pamoja na kupambana kuhakikisha anatimiza malengo.

“Pia nimejifunza kupenda kujaribu hususani yanapotokea mashindano mbalimbali ya ndani na hata nje ya nchi kama ilivyokuwa kwenye michuano ya Uturuki,” anasema.

Tayana ana elimu ya sekondari akiwa amehitimu kidato cha nne pia akiwahi kushinda taji la urembo katika Kitongoji cha Ukonga (Miss Ukonga mwaka 2009).

Tayana anaishauri Serikali pamoja na Chama cha Gofu Tanzania (TGU) kutoa kipaumbele kwa wanawake ili waweze kuleta mabadiliko na  kuutangaza vema mchezo huo kimataifa.

Mbali na hilo, anasema wajijengee utamaduni wa kukutana na wanawake katika klabu mbalimbali kuzungumzia changamoto zinazowakabili ili zipatiwe mwafaka.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -