Friday, October 23, 2020

TBF MMEONYESHA KWA VITENDO DHANA YA UWAJIBIKAJI

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

PONGEZI kubwa kwa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), kwa msimamo wenu mliouonyesha kuhakikisha michuano ya taifa mwaka huu inafanyika.

Pamoja na sintofahamu nyingi zilizojitokeza kwa wiki moja sasa juu ya kuwapo au kutokuwapo kwa mashindano hayo, TBF wamefanikiwa kusimama kuhakikisha kalenda yao ya mwaka inakamilika kwa kusogeza mbele kidogo  mashindano hayo.

Awali mashindano hayo yalipangwa kufanyika Desemba mosi mwaka huu, kabla ya kusogezwa hadi kesho ambapo yatafanyika katika Uwanja wa Soweto jijini Arusha.

Ni jambo la faraja kuona uongozi wa juu wa mchezo huo unapambana  kuhakikisha mashindano hayo  yanafanyika.

BINGWA tunaamani wadau wengi walisikia habari za kufanyika kwa mashindano haya kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii, hatua iliyoongeza hamasa kwa mikoa mbalimbali kujitokeza kuthibitisha ushiriki wao.

Wakati mikoa na timu zao zikijiandaa na safari kuelekea Arusha tayari kwa mashindano, ghafla zilitolewa taarifa za kusogezwa tarehe mbele kwa kile kilichodaiwa kuwa mdhamini kajitoa upande wa chakula.

BINGWA pia tunaushauri uongozi wa TBF kuhakikisha mnakuwa na  mawasiliano mazuri baina yenu na viongozi wa klabu za mikoa badala ya kutegemea taarifa za  vyombo vya habari na mitandao ya kijamii pekee kuwasiliana na wadau wenu.

Kanuni za mchezo huo nazo ni muhimu kuhakikisha timu na wachezaji kwa ujumla wanafanikisha malengo yao, hivyo upo ulazima kwa TBF kuweka kanuni za kueleweka na si za kubadilishwa yanapokaribia mashindano.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -