Monday, November 23, 2020

Tchetche akamilisha usajili Yanga

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA WAANDISHI WETU

BAADA ya figisu figisu za muda mrefu juu ya Yanga kumsajili mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche, hatimaye straika huyo amebakisha asilimia chache kabla ya kukamilisha usajili wake na kusaini mkataba wa kukipiga na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya Yanga, kililiambia BINGWA kuwa ipo mipango kabambe inayosukwa na vigogo matajiri wa Wanajangwani hao kuhakikisha Tchetche anarudi Tanzania na kukipiga kwa Wanajangwani hao na kwamba usajili wake unalengwa kufanikishwa kwenye dirisha dogo lililopangwa kufunguliwa Novemba 15 mwaka huu.

Mtoa habari wetu anasema licha ya Yanga kukamilisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni kwenye kikosi chao, bado wanaangalia uwezekano wa kuachana na mmoja wa wachezaji wao wa kimataifa ili kutoa nafasi kwa Kipre kuingia kikosini.

Pamoja na Kipre kupinga kutua Yanga akidai kutokuwa na mpango wa kucheza soka Tanzania baada ya kuondoka Azam, lakini kuna taarifa kuwa tayari ameshamalizana na Wanajangwani hao.

Mapema mwaka huu mwezi Mei, BINGWA lilinasa picha ya Kipre akionekana akisaini fomu akiwa nyumbani kwake Kijichi, kabla ya kuondoka kwenda kucheza soka la kulipwa barani Asia.

Taarifa za Kipre kutua Yanga, zinakuja ikiwa ni baada ya Wanajangwani hao kufanikiwa kumnasa kiungo wa Zesco, Mishek Chaila, ikiwa ni sehemu ya kukiimarisha zaidi kikosi chao ili kiweze kuwa katika ubora wa kuwawezesha msimu huu kutwaa ubingwa wa Bara kwa mara ya tatu mfululizo na kufanya vema kwenye anga ya kimataifa.

Juu ya suala zima la Kipre kusaini Yanga, BINGWA lilimtafuta mchezaji huyo na kuzungumza naye ambapo alikana kutua Jangwani akisema kuwa mipango yake hivi sasa amelenga zaidi kuisaidia timu yake Al-Nahda Al-Buraimi baada ya kuondoka Azam.

Katika hatua nyingine, vinara wa Ligi Kuu Simba nao wapo kwenye rada za straika huyo ambaye kwa sasa anakipiga kwenye klabu ya Al-Nahda-Buraimi ya nchini Oman.

Vigogo hao wa Simba, wamemtupia jicho Kipre kwenye usajili wa dirisha dogo huku kiungo wa timu hiyo, Musso Ndusha, akiwa kwenye hatihati za kuachwa.

Ndusha anaweza kuachwa kutokana na nafasi anayocheza kiungo huyo ina wachezaji wengi ndani ya kikosi hicho.

Tayari vigogo wa Simba wanaendelea na mazungumzo ya chini chini, ambapo inaelezwa kuwa ukaribu wake na kocha wa sasa, Joseph Omog, unatumika sana katika kutaka kufanikisha mpango wa kumleta nyota huyo.

Omog ambaye aliwahi kuipa Azam ubingwa, anatajwa sana kwenye ujio wa straika huyo kutokana na ukaribu wake alionao toka alipokuwa anafundisha kikosi cha Wanalambalamba.

Mwingine anayetajwa sana ni Katibu wa Simba, Patrick Kahemele ambaye naye aliwahi kufanya kazi Azam na kusaidia kwenye usajili wa Kipre na ndugu yake Michael Bolou.

Lakini yote kwa yote Azam pia wanataka kumrudisha mshambuliaji wao kutokana na timu ya Al-Nahda Al-Buraimi, Oman kutotoa fedha yoyote ya dau la uhamisho la mshambuliaji huyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -