Thursday, October 22, 2020

TFF IWEKE MIKAKATI YA KWENDA CAMEROON

Must Read

Wanaompenda Carlinhos wapewa dili

NA ASHA KIGUNDULA      MASHABIKI na wanachama wa Yanga, wakiwamo wale wanaovutiwa mno na uchezaji...

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

OKTOBA 12, mwaka huu, timu ya Taifa Stars itakuwa ugenini kucheza na Cape Verde katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika (Afcon), zitakazochezwa mwakani nchini Cameroon.

Baada ya mchezo huo wa Kundi L, Taifa Stars itarudiana na Cape Verde Oktoba 16, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

Tunatambua mchezo huo utakuwa ni mgumu kwa Taifa Stars, kwa kuwa wenyeji Cape Verde wanahitaji ushindi ili waweze kujiweka katika mazingira bora ya kufuzu fainali za mwakani.

Kutokana na Kundi L, Tanzania inasaka pointi sita katika michezo miwili itakayochezwa ugenini na nyumbani dhidi ya Cape Verde ili kuweza kufikia malengo ya kufuzu kwa mara nyingine fainali hizo, ambapo kwa mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1980, ambazo zilifanyika nchini Nigeria.

BINGWA tunaona mchezo kati ya Taifa Stars na Cape Verde hautakuwa rahisi kwa kuwa wenyeji hawatakubali kupoteza kwa mara nyingine baada ya mchezo wao wa kwanza kufungwa bao 1-0 na Uganda, kisha sare dhidi ya Lesotho.

Kwa maana hivyo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wana jukumu kubwa kuhakikisha wanaweka mipango kabambe ya kuiwezesha Taifa Stars kushinda katika michezo yote miwili.

Tunaamini kwamba mipango madhubuti ndiyo itakayowezesha Tanzania kuwa miongoni mwa timu zitakazokwenda kushiriki fainali hizo.

Tunasema kwamba, kwa muda uliobaki, TFF haitakiwi kulala usingizi wa pono, bali wafikirie jinsi watakavyomwezesha Kocha Mkuu wa timu hiyo, Emmanuel Amunike, kupata ushindi dhidi ya Cape Verde, baada ya hivi karibuni kutoka suluhu na Uganda katika Uwanja wa Taifa wa Mandela, Nambole, jijini Kampala.

Tunaamini kwamba, wachezaji wa Taifa Stars wakiongezewa sapoti na motisha, hakika wanaweza kufanya kile Watanzania wanachohitaji kwa muda huu, baada ya timu yao kushindwa kufuza fainali za Afcon kwa miaka mingi.

BINGWA tunaomba Watanzania wote kwa nafasi zao kujitokeza kuiunga mkono Taifa Stars ili iweze kufanya vizuri katika michezo ambayo inawakabili ya kuwania kufuzu fainali za Afcon.

Previous articleSIMBA WAANDAE UCHAGUZI HURU
Next articleKIBONZO
- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Wanaompenda Carlinhos wapewa dili

NA ASHA KIGUNDULA      MASHABIKI na wanachama wa Yanga, wakiwamo wale wanaovutiwa mno na uchezaji...

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote tatu katika mechi za Ligi...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na Staa Wako, safu inayokupa nafasi...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -