Monday, October 26, 2020

TFF wapangua tena ratiba VPL

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

NA ZAINAB IDDY

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepangua ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa ni mara ya tatu msimu huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF, mabadiliko hayo yamefanyika baada ya kupata tarehe rasmi za kalenda ya mechi za kirafiki za kimataifa ambazo timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itacheza.

Katika ratiba hiyo mpya iliyotolewa na Bodi ya Ligi na kusainiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wake, Boniface Wambura, inaonyesha kuwa mechi ya kiporo kati ya Yanga na Ruvu Shooting imepangwa kuchezwa Oktoba 26 mwaka huu.

Mechi nyingine ambazo awali hazikupangiwa tarehe kati ya Mwadui na Azam FC pamoja na Simba dhidi ya Tanzania Prisons zitacheza Novemba 9 wakati wa Ruvu Shooting ukichezwa Novemba 10 mwaka huu.

Mechi kati ya Yanga na Mtibwa Sugar iliyokuwa ichezwe Oktoba 12 sasa itapigwa Oktoba 13, huku mchezo wa  Kagera na Azam umesogezwa mbele kutoka Oktoba 28 hadi Oktoba 29.

Mchezo mwingine kati ya Yanga na Mbao FC, Toto Africans dhidi ya Mtibwa uliokuwa uchezwe Oktoba 29 umesogezwa mbele kwa siku moja, wakati mchezo wa Mtibwa Sugar na  Mbeya City na ule wa Majimaji na Mwadui itachezwa Novemba 7 mwaka huu badala ya Novemba 6 ya awali.

Mbali na mabadiliko hayo, mechi zote za Ligi Kuu ambazo zinaihusisha Azam FC zitakazochezwa Uwanja wa Chamazi Complex, sasa zitakuwa zikipigwa saa 1 usiku, hiyo ni kwa ajili ya kutoa fursa ya kibiashara kwa wadhamini, Azam TV.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -