Tuesday, January 19, 2021

TFF YAGAWA MIPIRA 100 ARUSHA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA JACKLINE LAIZER, ARUSHA

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limetoa mipira 100 kwa Chama cha Soka Mkoa wa Arusha (ARFA), kwa lengo la kuendeleza soka la vijana na wanawake hapa nchini.

Akizungumza wakati akikabidhi mipira hiyo kwa Katibu Mkuu wa ARFA, Zakayo Mjema wiki iliyopita, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF, Sarah Chao, alisema lengo la kugawa mipira ni kutaka kuzalisha vipaji vingi vya soka.

“TFF ina dhamira ya dhati ya kuona mpira unachezwa kuanzia ngazi ya chini, hivyo ninaomba mipira hii ikatumike kama ilivyolengwa ili tuweze kuzalisha vipaji vya baadaye, kwani tukiwekeza katika soka la vijana wenye umri mdogo tutaweza kufanikiwa zaidi,” alisema Sarah.

Kwa upande wake, Mjema alisema wao kama viongozi wa ARFA watahakikisha mipira hiyo wanaigawa kwa uwiano sawa katika vyama vya soka vya wilaya.

Mjema alisema vyama hivyo vitagawa mipira hiyo kwa vituo  vya kulelea vipaji chipukizi vya soka ‘Academy’ ili waweze kutimiza malengo ya shirikisho hilo.

“Kwa kweli ninaanza kuona mwanga wa mafanikio ya soka hapa mkoani kwetu, kama mnavyojua Mkoa wa Arusha ulivyodorora katika mchezo wa soka, tofauti na miaka ya nyuma ambapo mkoa huu ulikuwa wa kwanza kuwa na timu tatu zilizokuwa zinacheza Ligi Kuu.

Tulikuwa na timu ya AFC, JKT Oljoro na 977KJ, katika historia mkoa huu ndio chimbuko la soka la vijana hapa nchini,” alisema Mjema.

Katika hatua nyingine, Mjema alisema wanatarajia kufanya mkutano mkuu kwa kuwashirikisha viongozi mbalimbali wa soka la vijana mkoani hapa, ili kupanga mikakati ya kuweza kufanikiwa katika kuendeleza soka la vijana.

Mjema alisema mkutano huo  utapanga utaratibu wa kugawa mipira hiyo, iliyotolewa na shirikisho hilo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo Mkoa wa Arusha, ambaye ni Katibu Tawala (RAS), Richard Kwitega, alisema atahakikisha wanashirikiana bega kwa bega na uongozi wa ARFA kuhakikisha michezo, ikiwamo soka, inarudi katika kiwango chake kama miaka iliyopita.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -