Wednesday, October 28, 2020

TIGO FIESTA 2016 Weusi kukubali kufunikwa wakiwa kwao A Town?

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWANDISHI WETU,

BAADA ya mwishoni mwa wili iliyopita kukonga nyoyo za mashabiki wa burudani mkoani Kilimanjaro, hatimaye leo ni zamu ya wakazi wa Arusha ‘A Town’ na maeneo ya jirani kupata uhondo wa tamasha kubwa kabisa la burudani hapa nchini la Tigo Fiesta 2016.

Tamasha hilo la aina yake limezidi kutamba nchini na kutoa burudani katika mikoa mbalimbali ambapo baada ya kutikisa Kanda ya Ziwa, lilihamia Kanda ya Kati na hatimaye sasa likiwa Kanda ya Kaskazini.

Katika kanda hiyo, tayari mikoa ya Tanga na Kilimanjaro imeshapata mtikisiko wa tamasha hilo linalowahusisha wasanii wakali hapa nchini.

Katika tamasha hilo, wapenzi wa muziki wamejikuta wakipata burudani safi kutoka kwa wasanii mbalimbali ambao wamefanikiwa kutoa shoo ya aina yake.

Wasanii ambao wamekuwa wakipanda jukwaani katika mikoa yote tamasha hilo lilikofanyika, wameacha gumzo kutokana na burudani ya nguvu waliyoitoa, kuanzia katika uimbaji hadi uchezaji.

Lakini pia kwa mwaka huu wasanii wameonesha uwezo mkubwa wa kuimba muziki wa moja kwa moja wakiwa kwenye majukwaa tofauti na ilivyokuwa misimu kadhaa iliyopita.

Burudani hiyo kwa mwaka huu imekwenda sambamba na ugawaji wa madawati kutoka kampuni ya Tigo kwa kila mkoa ambao tamasha hilo limefanyika.

Kuelekea tamasha la leo, wasanii watakaopanda jukwaani wameahidi shoo ya aina yake ili kukonga nyoyo za wakazi wa mji huo na maeneo ya jirani.

Mmoja wa wasanii watakaopanda jukwaani leo ni Bernard Paul ‘Ben Pol’ ambaye ametamba kufanya mambo makubwa na kuacha gumzo mkoani humo kama ilivyokuwa katika mikoa waliyopitia.

Akizungumzia shoo hiyo, Ben Pol anasema kuwa amejipanga vilivyo kuhakikisha anakonga nyoyo za mashabiki zake na wapenda burudani kwa ujumla.

Anasema kuwa kama kawaida yake, atafanya vitu tofauti kabisa na vile vilivyozoeleka, kama sehemu ya kuwaonyesha mashabiki wake ni kwa kiasi gani anawajali.
“Shoo zangu mwaka huu zipo tofauti kidogo na ilivyokuwa katika kazi zangu zilizopita, kuanzia uimbaji, mpangilio wa muziki na mwonekano wake,” anasema Ben Pol ambaye amekuwa ni mmoja wa wasanii walionufaika mno na Tigo Tanzania ambao wamekuwa wakimpiga jeki katika kazi zake nyingi.

Mbali ya Ben Pol, wasanii wanaounda kundi la Weusi, wakiongozwa na mkali, Joh Makini, leo wakiwa katika mkoa wao, wanatarajiwa kufanya mambo makubwa ili kuepuka kufunikwa na wenzao.

Na kwa kuwa watakuwa mbele ya mashabiki wao, ni ukweli usiopingika kuwa wanatarajiwa kupata sapoti ya nguvu kuanzia katika kuimba hadi kucheza nyimbo zao.

Hata hivyo, akina Joh Makini watatakiwa kuwa makini hasa kwani wasanii wengineo waliobahatika kuwapo katika orodha ya watumbuizaji wa Tigo Fiesta 2016, wameonekana kujipanga vilivyo kama ilivyojidhihirisha katika mikoa ambayo tamasha hilo ‘limeacha vumbi’.

Miongoni mwa wanaotarajiwa kutoa upinzani kwa Weusi leo, ni mtaalamu wa nyimbo za mapenzi, Ben Pol, kundi la Navy Kenzo, Man Fongo, Snura na wengineo. Je, Weusi watakubali kufunikwa leo? Tusubiri tuone kama si kusikia.

Mbali ya hao, wasanii wengineo wanaotarajiwa kupanda jukwaani leo ni Jux, Christian Bella, Mr Blue, Vanessa Mdee, Darassa, Baraka da Prince, Dully Sykes, Fid Q, Chege, Maua, Linah, Nandy, Moni na Bonge la Nyau.

Waandaaji wa Tamasha la Fiesta, Kampuni ya Prime Times Promotion chini ya Mkurugenzi Mtendaji wake, Joseph Kusaga, wameahidi tamasha la mwaka huu likiwa ni la 15 kuwa la aina yake katika kila mkoa watakaofika na kwamba wapenzi wa burudani watarajie kupata shoo za nguvu kutoka kwa wasanii wao.

Kusaga, anasema: “Tutaendelea na harakati zetu za kuendeleza vipaji kutoka kwa wasanii wapya na wanaoibukia katika kizazi kipya wakati wa tamasha la Fiesta 2016 kama ambavyo tulifanya awali wakati wa tamasha la Dance la Fiesta, Fiesta Super Star na Bonanza la Soka la Fiesta.

“Ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 15 ya tamasha la Fiesta nchini, mwaka huu tutaendesha kampeni maalum inayojulikana kama ‘kipepeo’ kwa ajili ya kuwatambua na kuwasaidia wasichana walio na mahitaji maalumu katika mikoa 15 ambako tamasha  hili litafanyika.”

Kwa upande wake, Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Savkat Berdiev, anasema wapenzi wa muziki watarajie burudani ya nguvu kutoka kwa wasanii wa muziki wa ndani na nje ya nchi.

“Ikiwa ni kampuni iliyojikita katika kukuza sekta ya muziki wa ndani, tunayo furaha kuwa wadhamini wakuu wa tamasha hili kubwa la muziki nchini Tanzania. Lengo letu kila mara limekuwa ni kunyanyua wasanii wa ndani kupitia majukwaa ambayo  yatawawezesha kuonesha vipaji vyao, kuwaunganisha na  mashabiki ili kuzipaisha  kazi zao na kufanikiwa kupata kiasi kikubwa cha fedha,” anasema.

Akielezea zaidi jinsi mashabiki wa muziki nchini na wateja wao wanavyonufaika na tamasha la mwaka huu, Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga, anasema wanawapatia vifurushi vinavyowawezesha kuchagua kati ya data za GB 1 au visivyo na ukomo vinavyojumuisha dakika 490 Tigo kwenda Tigo.

“Tamasha la Fiesta linawakaribisha Watanzania wote na pia tukio hili linatoa shuguli za kijamii tukiwa na kauli mbiu yetu Fiesta 2016 kwa Kishindo cha Tigo Imoooo,” anasema Mpinga.

Baada ya tamasha hilo kunguruma Arusha leo, wiki ijayo itakuwa ni zamu ya Mtwara kabla ya kuhamia Iringa, Mbeya na kumalizikia Dar es Salaam.

Mashabiki wa Arusha wanaweza kupata tiketi zao kwa njia ya Tigo Pesa na kwa kufanya hivyo, wanapata punguzo ya asilimia kumi kwa kuwa watanunua kwa Sh 9,000, wakati wakikata tiketi mlangoni inakuwa Sh 10,000.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -