Wednesday, October 21, 2020

TIGO FIESTA 2018… WEUSI, NANDY, CHEGGE KUITEKA SUMBAWANGA

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA MWANDISHI WETU


 

BAADA ya kutimua vumbi kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Jumamosi iliyopita, tamasha la Tigo Fiesta 2018-Vibe Kama Lote wikiendi hii linahamia mjini Sumbawanga, huku wasanii wa kundi la Weusi wakiongozwa na mkali, Joh Makini, wakitarajiwa kuongoza mashambulizi.

Mji wa Morogoro ndio uliopata bahati ya kufungua Dimba msimu wa Tigo Fiesta wa 2018, huku kaulimbiu ikiwa ni ‘Vibe Kama Lote’, ambapo wasanii waliopanda jukwaani walifanya shoo ‘bab-kubwa’ iliyoacha gumzo miongoni mwa maelfu ya mashabiki waliofurika kushuhudia burudani hiyo ya kila mwaka.

Katika shoo hiyo iliyofunguliwa saa 12 jioni, wasanii wanaochipukia kutoka Morogoro wakiongozwa na washindi, Supa Nyota kimkoa, Michael Yusufu ‘Belly 255’ na Abdul Michael ‘V Dax’, walishiriki shindano la kusaka vipaji la Tigo Fiesta 2018 – Supa Nyota.

Shangwe zaidi zililipuka wakati kundi linalokuja kwa kasi la Mesen Selekta pamoja na msanii WhoZu anayetambaa na wimbo wake wa Huendi Mbinguni, walipopanda jukwaani na kusababisha vumbi kutifuka miongoni mwa mashabiki.

Wasanii wengine waliokonga nyoyo za mashabiki siku hiyo ni wale wa Kundi la Rostam linaloundwa na Roma pamoja na Stamina, huku Fid-Q aliyeambatana na msanii wa kike wa muziki wa kufokafoka, Rosaree, Ben Pol, Mr Blue ‘Kabayser’, Dogo Janja, Maua Sama, Nandy na Belle 9 nao wakifanya yao.

Wasanii wote walionesha uwezo mkubwa wa kuimba na kumiliki jukwaa, huku wote wakiwa wamejiandaa kikamilifu pamoja na wacheza dansi waliokuwa wamevalia sare za kuvutia.

Katika hali ambayo haikuwa imetegemewa na wengi, msanii mkongwe wa Bongo Fleva ambaye ni Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Professor Jay’, aliambatana na wasanii wengine wakongwe, akiwamo Black Rhino na kufanya shoo ya kukata na shoka na kuwafanya hata wale waliokuwa wameanza kutoka uwanjani, kurudi ndani na kukesha hadi alfajiri.

Akizungumzia tamasha la Sumbawanga, Katibu Mkuu wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardner G. Habash, aliwahakikishia burudani ya hali ya juu wote watakaohudhuria tamasha hilo mjini humo.

Mbali na Kundi la Weusi, Habash aliwataja wasanii wengine watakaopanda jukwaani mjini Sumbawanga wikiendi hii kuwa ni Maua Sama, Chegge, Bilnass, WhoZu, Marioo, Nedy Music, Barnaba, Fid Q, Ben Pol, Nandy wengineo wa mjini humo.

Katika miaka ya hivi karibuni, tumetambua mchango mkubwa wa kiuchumi na kijamii unaotokana na tamasha la Tigo Fiesta. Mbali na kutoa fursa ya kuutangaza mkoa husika, pia inaongeza idadi ya wageni na kusababisha ongezeko kubwa la fursa za biashara kwa wamiliki wa hoteli, migahawa, mama nitilie, vyombo vya usafiri kama vile bodaboda, kumbi za starehe na biashara nyinginezo,” alisema Habash.

Kwa upande wake, Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga, alisema: “Tigo inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia TigoPesa Masterpass QR. Tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa TigoPesa Masterpass QR zitagharimu Sh 5,000 pekee badala ya Sh 7,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslim.

“Wateja wanapaswa kupiga *150*01#  na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.”

Mpinga aliongeza: “Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 –Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za Sh 100,000, zawadi za kila wiki za Sh milioni moja, simu janja za mkononi zenye thamani ya Sh 500,000 kila moja pamoja na donge nono la Sh milioni 10 kwa mshindi wa jumla.

“Kushiriki, wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya  http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.”

Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta, ambapo mwaka huu litashirikisha asilimia 100 ya wasanii wa nyumbani watakaozuru mikoa 15 ya nchi.

Baada ya Morogoro na Sumbawanga, maeneo yatakayofuata ni Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele kikifanyika jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -