Tuesday, October 27, 2020

TIGO FIESTA 2018…Dogo Janja, Rosa Ree, Mavoko kuongoza mashambulizi Moshi

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWANDISHI WETU

TAMASHA la burudani la Tigo Fiesta 2018-Vibe Kama Lote, wikiendi hii linahamia Kanda ya Kaskazini, ikiwa ni baada ya kuacha vumbi katika mikoa ya Ruvuma kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea na Mtwara Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Mbali na Songea na Mtwara, hadi sasa tamasha hilo limesharindima katika miji ya Morogoro, Sumbawanga na Iringa.

Kwa upande wa Kanda ya Mashariki, tamasha la kila mwaka, kesho litafanyika mjini Moshi kabla ya Jumapili hii kutimua vumbi Jiji la Tanga.

Wakazi wa Moshi wanatarajiwa kupata ladha tofauti na ile waliyoionja wenzao wa Songea na Mtwara kwani ‘macharii’ hao wameongezewa uhondo wa burudani kutoka wa wakali wa muziki hapa nchini, Rich Mavoko, kijana kutoka Arusha, Dogo Janja ‘Janjaro’ na binti mwenye kipaji cha hali ya juu katika hip hop, Rosa Ree.

Ikumbukwe kuwa wasanii hao watatu hawakuwapo katika matamasha yaliyofanyika Songea na Mtwara, hivyo wakazi wa Moshi na hata Tanga watarajie burudani iliyokwenda shule.

Katika matamasha ya Songea, Mtwara na kwingineko ulikopita uhondo huo, wasanii walifanya shoo ya nguvu iliyokonga nyoyo za wapenzi wa muziki na burudani kwa ujumla.

Wasanii wote walionesha uwezo mkubwa wa kuimba na kumiliki jukwaa, huku wakionekana kujiandaa kikamilifu kuwapa burudani ya nguvu Watanzania kama ilivyo kawaida ya tamasha hilo la kila mwaka linaloratibiwa na Kampuni ya Clouds Media.

Akizungumzia tamasha la Moshi, Katibu Mkuu wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardner G. Habash, aliwahakikishia burudani ya hali ya juu wote watakaohudhuria tamasha hilo mjini humo.

Mbali na Rich Mavoko, Janjaro na Rosa Ree, Habash aliwataja wasanii wengine watakaopanda jukwaani mjini Moshi kesho kuwa ni Rostam, WhoZu, Chid Benz, Maua Sama, Chegge, Nandy, Mr Blue na  wengineo wa mjini humo.

“Katika miaka ya hivi karibuni, tumetambua mchango mkubwa wa kiuchumi na kijamii unaotokana na tamasha la Tigo Fiesta. Mbali na kutoa fursa ya kuutangaza mkoa husika, pia inaongeza idadi ya wageni na kusababisha ongezeko kubwa la fursa za biashara kwa wamiliki wa hoteli, migahawa, mama nitilie, vyombo vya usafiri kama vile bodaboda, kumbi za starehe na biashara nyinginezo,” alisema Habash.

Kwa upande wake, Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga, aliwataka wapenzi wa burudani wa Moshi na maeneo ya jirani, kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo ili kupata burudani ya nguvu kutoka kwa wasanii wao wa nyumbani.

Mpinga aliongeza: “Tigo inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa Tigo Pesa Masterpass QR zitagharimu Sh 5,000 pekee badala ya Sh 7,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslim.

“Wateja wanapaswa kupiga *150*01#  na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.”

Mpinga alisisitiza: “Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018–Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za Sh 100,000, zawadi za kila wiki za Sh milioni moja, simu janja za mkononi zenye thamani ya Sh 500,000 kila moja pamoja na donge nono la Sh milioni 10 kwa mshindi wa jumla.

“Kushiriki, wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya  http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.”

Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta ambapo mwaka huu litashirikisha asilimia 100 ya wasanii wa nyumbani watakaozuru mikoa 15 nchini.

Baada ya Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Songea, Mtwara na Moshi, maeneo yatakayofuata ni Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele kikifanyika jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -