Wednesday, October 28, 2020

TIMU IPI ITAMFAA RODRIGUEZ ?

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MADRID, Hispania

JAMES Rodriguez hana furaha na maisha ya Madrid kwa sasa, kumbuka zile nyakati za kuufurahia mchezo wa soka alizokuwa nazo pale AS Monaco, Ufaransa kabla ya kutua Real Madrid. Na sasa anataka kuondoka katika dirisha la usajili litakalofunguliwa wiki chache zijazo.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Colombia, bado anatambulika kama kiungo mshambuliaji bora wa soka la kisasa, ingawa nafasi yake kwenye kikosi cha kocha Zinedine Zidane imekuwa finyu katika siku za hivi karibuni.

Baada ya kutoka kwa taarifa kwamba anataka kutimka Januari mwakani, lakini Arsenal na Manchester United pia ziliwahi kuhusishwa naye na bado zipo kwenye orodha ya wanaomwania.

Kutokana na hilo, makala hii imechambua ni klabu ipi itakayomhitaji zaidi Rodriguez na nafasi ipi atakayong’ara?

 Manchester United

United haina upungufu mkubwa wa viungo washambuliaji kwa kipindi hiki, lakini kama Rodriguez akitua na kucheza kwa kiwango cha hali ya juu, watu kama Wayne Rooney, Jesse Lingard, Anthony Martial au Marcus Rashford itabidi wamsubirie benchi tu.

Rodriguez, mwenye umri wa miaka 25, ni mzuri achezapo pembeni au katikati, lakini namba 10 ndiyo nafasi inayotakiwa kuongezwa nguvu pale United kwa ajili ya kumpa sapoti ya kutosha Zlatan Ibrahimovic.

Hata hivyo, haitakuwa kazi nyepesi kwa Rodriguez kufanya vyema kwa muda mfupi atakaoishi England kutokana na ugumu wa ligi husika, kwa upande mwingine, je, usajili huu utaweza kuwapa United changamoto nyingine iwapo ni mchezaji anayefanana na mifumo ya Mourinho kwa wakati ambao Paul Pogba naye anaendelea kuzoeshwa presha ya kikosi kinachosubiriwa kufanya makubwa miaka ya mbeleni?

 Arsenal

Ndani ya klabu hii, Rodriguez atafanya vyema kwenye upande wa kushoto kutokana na vijana Alex Iwobi na Alex Oxlade-Chamberlain kutoonesha nguvu yao ya kuutumikia upande huo.

Unaweza kudhani labda hatafanya vizuri upande huo, lakini kwa mfumo wa soka la pasi fupi fupi za haraka pamoja na uwepo wa Mesut Ozil, Rodriguez atang’ara vilivyo.

Kwa changamoto ya majeruhi inayoikumba Arsenal, Rodriguez atakuwa msaada, lakini pindi mambo yanapokuwa magumu ndani ya mechi kubwa baadhi ya wachezaji wanaotegemewa hupotea ghafla na hili litaweza kuathiri kiwango cha Rodriguez pia kama Zidane anavyolalamika pale Madrid kuwa Mcolombia huyo si mpambanaji haswa.

Je, Wenger, ambaye anapenda kuwa na mchezaji anayejua majukumu ya uongozi uwanjani, atamhitaji?

 Chelsea

Ndani ya timu hii, inaweza kupatikana nafasi kwa Rodriguez na Kocha Antonio Conte ni lazima atahitaji kikosi kipana kitakachopambana vilivyo msimu huu, ukizingatia mtindo wake wa kutumia kikosi kimoja kila mechi.

Kwa sasa Willian na Pedro wanafanya vizuri upande wa kulia, wakipokezana nafasi mechi na mechi na iwapo Rodriguez atatua Stamford Bridge, ni wazi atakuwa msaada kwa Chelsea chini ya uangalizi wa Conte.

Kiungo huyo wa zamani wa Monaco atakuwa ni mchezaji huru ndani ya mfumo wa Conte kama Eden Hazard anavyotamba msimu huu, huku akipata ulinzi wa kutosha kutoka kwa Victor Moses.

Chelsea wanaweza kuonekana kama vile hawamhitaji, lakini kulingana na pengo litakaloachwa na Oscar (upana wa kikosi) ni wazi matajiri hao wa London watamwaga fedha kusaka mchezaji muhimu Januari.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -