Friday, October 23, 2020

TIMU NDOGO KUWENI MAKINI NA ‘MAFAZA’ MNAOWAPOKEA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA HASSAN DAUDI

DIRISHA la usajili linatarajiwa kufungwa Desemba 15. Ni siku tatu pekee zimebaki kabla ya kufikia tamati kwa mchakato huo.

Kwa kipindi chote hiki cha usajili, mashabiki wa soka wameshuhudia uhamisho wa wachezaji mbalimbali.

Wapo waliohama kutoka timu moja kwenda nyingine lakini pia kuna idadi kubwa ya mastaa walioongeza mikataba ya kuendelea kukipiga katika klabu zao za zamani.

Tumeshuhudia ujio wa wachezaji wa kimataifa katika klabu kadhaa zilizomudu kufanya hivyo. Ndiyo, si kila timu ina uwezo wa kuzinasa saini za mastaa kutoka nje ya nchi.

Binafsi, nategemea upinzani mkali wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara katika mzunguko wa pili utakaoanza kutimua vumbi Desemba 17.

Hata hivyo, kuna jambo moja la hatari limekuwa likiendelea kufanyika tangu kufunguliwa kwa dirisha hili dogo la usajili ambalo barani Ulaya litaanza mwezi ujao.

Bado kumekuwa na tabia ya timu ndogo kubabaikia wachezaji wakongwe wanaoachwa na klabu kubwa.

Tumeshuhudia timu nyingi ambazo mara nyingi ni zile zinazopambana kubaki ligi kuu zikihaha kuwapokea mastaa wanaotemwa na klabu maarufu za Simba, Yanga na Azam.

Imekuwa ni sifa kwa timu ndogo kuwa na idadi fulani ya wachezaji wa zamani wa klabu hizo zenye heshima kubwa katika soka la hapa nchini.

Viongozi wa timu hizo wamekuwa wakipambana na kuhakikisha wanazinasa huduma za wachezaji hao ikiwa ni imani yao kuwa uzoefu wao utazisaidia timu zao.

Hata hivyo, kwa kipindi kirefu nimekuwa nikifuatilia sula hilo na kugundua kuwa timu ndogo zimekuwa zikihadaika na majina makubwa waliyonayo mastaa hao.

Kwa utafiti wangu mdogo, nimeibuka na jibu kuwa timu hizo zimejikuta zikitumia fedha nyingi kuwasajili mastaa hao huku zikiumia zaidi kuwalipa mishahara minono.

Tofauti ya matarajio ya timu hizo, mara nyingi ‘mafaza’ hao wamekuwa mzigo mkubwa kwao.

Idadi kubwa ya wachezaji hao wanaoachwa na timu kubwa huwa wamechoka. Huku wengine umri ukiwa umewatupa mkono, wapo ambao viwango vyao huwa vimeshuka kwa kiasi kikubwa.

Wengi huwa wamekaa benchi kwa kipindi kirefu katika klabu walizotoka, hivyo itawachukua muda mrefu kurejesha makali yao na kuweza kuwa msaada kwa timu ndogo.

Hivi unakumbuka kilichomkuta kocha mwenye maneno mengi hapa nchini, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’?

Sote tunamjua Julio, hasa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufundisha soka. Ni mmoja kati ya makocha ambao Tanzania inaweza kujivunia kokote ulimwenguni.

Mara nyingi huwa sioni tofauti yake na Jose Mourinho, ni makocha wanaojua mbinu za kupata ushindi kwa nmna yoyote ile.

Huenda wengi hawajui kilichomwagusha Julio pale Mwadui. Ni hiki ninchokizungumzia hapa, kubabaikia wachezaji waliotemwa na klabu zenye majina makubwa.

Wengi tulitarajia Mwadui ingekuwa moja kati ya timu tishio kwa vigogo hapa Bongo. Wapo walioanza kujenga ‘top four’ ya VPL ambayo ilizijumuisha Simba, Yanga, Azam na Mwadui.

Nilianza kuhisi anguko la Julio na Mwadui yake pale tulipoanza kusikia kikosi chake kikiundwa na mastaa wengi waliotoka klabu kongwe.

Sikutaka kujiridhisha na kile nilichokuwa nikiamini kabla ya ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita.

Nilianza kuifuatilia Mwadui kuanzia mwanzo wa ligi na ndipo nilipoamini kuwa nilichotabiri kilikuwa sahihi.

Kiasi kikubwa cha fedha kilichotumiwa na timu hiyo ya jijini Shinyanga kuwasajili nyota hao, hakikuendana na kile walichokuwa wakikifanya uwanjani.

Nilichoweza kukibaini ni kwamba wachezaji wasiokuwa na majina ndiyo waliokuwa wakijitoa zaidi uwanjani, kuliko mafaza hao ambao wengi walionekana wakitembea tu kwa dakika zote za mchezo.

Kilichofuata ni Julio kubwaga manyanga huku kisingizio chake kikubwa kikiwa ni utendaji mbovu wa waamuzi wa VPL.

Ambacho Julio alishindwa kukiweka wazi ni kuwa mafaza aliowasajili walishindwa kumrahisishia kazi na badala yake walikuwa mzigo wa misumari kwake.

Lakini pia, mara nyingi mafaza hao hujiunga na timu ndogo wakiwa na ‘pancha’ za kudumu.  Kwa majanga hayo, hujikuta wakitumia muda mrefu wakiwa nje ya uwanja kuuguza majeraha yao kuliko kuisaidia timu kupiga hatua.

Ikumbukwe kuwa kumekuwa na utamaduni wa timu kubwa kushindwa kuhudumia wachezaji wao vizuri pindi wanapopata majeraha, hivyo huwaacha wanapohisi watakaa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.

Hata hivyo, si wachezaji wote wanaotemwa na timu kubwa huwa ‘wamefulia’. Wapo wanaoachwa kutokana na ‘figisufigisu’ za soka la hapa Bongo. Eti hata msemaji wa timu ana uwezo wa kumfukuza mchezaji kikosini! Naomba kuwasilisha!

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -