Sunday, January 17, 2021

TOURE ANAIPENDA MAN CITY AU AMESHIBA FEDHA?

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

MANCHESTER, England

NTOTA Yaya Toure ameonyesha kuwa fedha si kila kitu katika maisha yake. Amethibitisha kuwa kipaji chake cha soka ni zaidi ya fedha.

Staa huyo Mwafrika raia wa Ivory Coast, amekataa dili la kujiunga na moja ya klabu tajiri ya Ligi Kuu nchini China ambayo ilikuwa tayari kumlipa mshahara wa kitita cha pauni 430,000 (zaidi ya Sh bilioni moja za Kitanzania).

Ikumbukwe kuwa mastaa wa Ligi Kuu England ambao hivi karibuni walitimkia China, ni pamoja na viungo Oscar na John Mikel Obi wa Chelsea.

Lakini pia, mchezaji wa zamani wa Manchester United na Man City, Carlos Tevez, naye ametua katika klabu ya Shanghai Shenhua, ambapo amekuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi duniani.

Mpachikaji mabao hatari wa Blues, Diego Costa, naye anatajwa kuwaniwa na Tianjin Quanjian, klabu ambayo wiki kadhaa zilizopita ilimsajili Axel Witsel.

Imeelezwa kuwa Tianjin walikuwa tayari kumlipa Costa mshahara wa pauni milioni 15 lakini sheria mpya za Chama cha soka nchini humo kilikwamisha mpango huo.

Chama hicho kimeweka sheria inayozuia timu moja kuwa na idadi kubwa ya mastaa wa kigeni, ikisisitiza zaidi uzalendo kutoa nafasi kwa wachezaji wazawa.

Ni wachezaji watatu pekee kutoka nje ya China wanaoweza kuingia uwanjani kwenye mchezo mmoja.

Toure amesisitiza kuwa mpango alionao ni kuendelea kukipiga katika klabu ya Manchester City na si kutimkia barani Asia.

Kiungo huyo anakataa mshahara huo mnono wa pauni 430,000, huku akiwa analipwa pauni 220,000 tu kwa mwaka pale Man City.

Kwa sasa ana umri wa miaka 33 na huenda hiyo ilikuwa ofa nono zaidi katika maisha yake ikiwa tayari ameanza kuoneakana ‘babu’. Ni ngumu kutabiri kuwa atapata dili kama hilo miaka mitano ijayo.

Hata hivyo, Toure ameamua kukataa mshahara huo kwa kuwa tayari ameshatengeneza utajiri wa dola za Marekani milioni 70 au ni kweli anaipenda Man City ambayo haionekani kumjali?

Pia, anakamata nafasi ya tatu kwa wanasoka wa Afrika wenye mkwanja mrefu. Anayeongoza ni Samuel Eto’o na Didier Drogba anakamata nafasi ya tatu.

Toure amekuwa akitajwa kuwaniwa na klabu za China kwa klipindi kirefu na mfano mzuri ni kipindi kile cha usajili cha majira ya kiangazi cha mwaka jana.

Aliupuuzia mpango huo na sasa Wachina wameonekana kupanga kukamilisha dili hilo kabla ya Januari 31, siku ambayo dirisha hili dogo la usajili litafungwa.

Mkataba wa sasa wa Toure na mabosi wake wa Etihad utafikia tamati majira ya kiangazi.

Kwa upande mwingine, bado hakuna mazungumzo ya mkataba mpya yanayoendelea kati ya nyota huyo na Man City.

Kwa mantiki hiyo, kuna uhakika kuwa ataendelea kubaki klabuni hapo au atafungasha virago vyake na kutimkia kwingineko.

Lakini pia, ingawa kwa sasa hali imeonekana kuwa shwari, kumekuwa na uhusiano mbovu kati yake na kocha raia wa Hispania, Pep Guardiola, ambaye ndiye anayeinoa Man City kwa sasa.

Itakumbukwa kuwa mwanzoni mwa msimu huu, Guardiola alimsugulisha benchi Mwafrika huyo kabla ya kumrejesha kikosini katika siku za hivi karibuni.

Lakini pia, Guardiola amekuwa aking’ata maneno kila anapoulizwa juu ya hatima ya Toure pale Etihad licha ya ukweli kwamba amekuwa akimtumia mara kwa mara katika michezo ya hivi karibuni.

Kwa mujibu wa sheria, hivi sasa Toure yuko huru kusaini mkataba wa awali na klabu yoyote, lakini ameonyesha kupuuzia mpango wa kuondoka Man City.

Amesisitiza kuwa bado analipenda soka la England, hasa klabu yake ya Man City.

Bado uongozi wa Man City haujamhakikishia Toure nafasi yake ya kuendelea kuichezea timu hiyo.

Staa huyo alijiunga na Man City mwaka 2010 na amekuwa sehemu muhimu ya safu ya kiungo tangu Mjerumani Ilkay Gundogan alipoumia goti.

Tangu Gundogan alipoumia Desemba 14 katika mchezo dhidi ya Watford, Toure amekuwa akiingia uwanjani mara kwa mara.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -