Monday, August 10, 2020

TP Mazembe yaifanyia umafia Simba

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

MWANDISHI WETU

KLABU ya TP Mazembe ya DR Congo, imeifanyia umafia Simba kwa beki mahiri asiyecheka na mtu awapo uwanjani, Kabaso Chongo, baada ya kumpa mkataba mpya fasta mara waliposikia mchezaji huyo yupo njiani kutua Msimbazi.

Habari kutoka ndani ya TP Mazembe, zinasema kuwa awali klabu hiyo ilikuwa haina papara na beki huyo, wakiamini ataendelea kuwa mali yao.

Mtoa habari wetu ameliambia BINGWA jana kuwa wakati viongozi wa TP Mazembe wakiendelea ‘kula bata’, walidokezwa kuwa Chongo tayari amefanya mazungumzo na Simba, ndipo waliposhtuka na kumpa mkataba mpya wa miaka miwili fasta.

Lakini kwa kuwa Simba walionekana kuhitaji beki wa kati kwa udi na uvumba wa kiwango cha juu, mmoja wa mameneja anayeshusha vifaa Msimbazi, amewatafutia mwingine moto wa kuotea mbali.

Beki huyo anakwenda kwa jina la Mukombozi Derrick anayekipiga katika kikosi cha Rukinzo FC ya Ligi Kuu Burundi.

“Awali Kabaso alishamaliza na na Simba, kilichokuwa kimebaki ilikuwa ni kuja huko Tanzania kusaini mkataba tu, lakini Mazembe waliposikia hilo, walimuita mezani haraka na kumpa mkataba mpya mnono.

“Kuona hivyo, meneja ambaye amekuwa akiwaletea Simba wachezaji wengi tu wanaofanya vizuri, amewatafutia beki mwingine kutoka klabu ya Rukinzo FC anayejulikana kwa jina la Derrick na tayari wameshaanza mazungunzo, naamini huyu ndiye atakayechukua nafasi ya Kabaso,” alisema mtoa habari wetu huyo.

Derrick ana nafasi kubwa ya kutua Simba kwani kutokana na kuwa na umri wa miaka 28, Wekundu wa Msimbazi hao wanaamini atawasaidia kwa muda mrefu zaidi.

Inafahamika kuwa Simba inasaka beki mzoefu wa kiwango cha Pascal Wawa, lakini mwenye umri kati ya miaka 26 hadi 29 ili kuiimarisha safu yao ya ulinzi.

Wawa na Erasto Nyoni waliokuwa wakicheza pamoja kama mabeki wa kati Simba, wanaonekana umri kuwatupa mkono hivyo kasi yao kuanza kupungua, huku Kennedy Juma akiendelea kuimarika, akipata uzoefu kutoka kwa ‘kaka’ zake hao.

Mbali ya beki, Simba inasaka mshambuliaji wa kati mzoefu na mwenye uchu wa mabao wa kusaidiana na Meddie Kagere na John Bocco.

Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara, msimu ujao wanashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wakiwa wamepania kufika mbali baada ya msimu huu kuishia hatua ya awali.

Msimu uliopita, Simba ilifika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa kabisa kwa ngazi ya klabu barani Afrika.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -