Wednesday, October 28, 2020

TPLB YATOA UFAFANUZI MDHAMINI LIGI KUU

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA WINFRIDA MTOI


BODI ya Ligi Tanzania (TPLB), imeweka wazi kwamba Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao itaanza bila kuwa na mdhamini mkuu wakati wakiendelea na mazungumzo na makampuni kadhaa ili yaidhamini ligi hiyo.

Awali ligi hiyo ilikuwa ikidhaminiwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, ambayo mkataba wake umemalizika na tayari wameanza mazungumzo, lakini hadi sasa hawajafikia makubaliano.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPLB, Boniface Wambura, alisema wameamua kufanya hivyo kutokana na kalenda yao ya mashindano kuwabana.

Alisema kalenda ya ligi kulingana na mashindano mengine inatakiwa kuanza kuanza Agosti 22, mwaka huu na wameshawasiliana na klabu kuwa wanaendelea na mazungumzo na mdhamini mkuu.

Aidha, Wambura alisema kati ya kampuni wanazozungumza nazo ni pamoja na mdhamini aliyemaliza mkataba wake, Vodacom na watakapofikia makubaliano muda wowote watatoa taarifa kwa klabu.

“Tunaanza ligi, lakini ifahamike kuwa mdhamini mkuu hatakuwapo, pia kampuni tunazofanya nazo mazungumzo tumekubaliana wataingia katikati mara tutakapofikia mwafaka, waliopo kwa sasa, Benki ya KCB na Azam TV ni wadhamini wenza,” alisema Wambura.

Hata hivyo, alikiri kwamba ligi kuanza bila kuwa na mdhamini mkuu itakuwa na changamoto, lakini tayari wamezipa taarifa klabu kutokana na hali hiyo, hivyo hata vifaa zitajigharamia zenyewe.

“Kwa sasa ligi itaitwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na hata jezi za timu pale inapokaa nembo ya mdhamini mkuu patabaki wazi, tunajua kuna changamoto ya kifedha, lakini tunazihakikishia klabu mdhamini mkuu atapatikana,” alisema Wambura.

Katika hatua nyingine, TFF kwa kushirikiana na Bodi ya Ligi imerejesha mfumo wa tiketi za wanafunzi katika mechi za Ligi Kuu msimu ujao unaotarajiwa kuanza Agosti 22, mwaka huu.

Akizungumzia uamuzi huo, Wambura alisema unalenga kutoa nafasi kwa vijana kuangalia mpira na wamefanya hivyo kutokana na programu zao za kuwahamasisha kwa kuwapa nafasi za kushuhudia ligi kwa kulipa nusu kiingilio.

Aidha, alisema tiketi hizo zinawalenga hasa wanafunzi wa shule za sekondari kwa sababu ili kuzitumia lazima uwe na kitambulisho cha shule unayosoma.

“Hizi tiketi zilikuwapo kipindi cha FAT (Chama cha Soka Tanzania) zikaondolewa, lakini msimu ujao zitarudishwa, mfumo huu pia utaepusha usumbufu kwa wale wanaokuja na watoto uwanjani, kwani watakuwa na jukwaa lao maalumu,” alisema Wambura.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -