Monday, November 23, 2020

TRA SASA MTUWEKE WAZI KUHUSU KODI HII MNAYOIDAI TFF

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA IRINE MPATWA, OUT

JUZI Mawakala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), walikamata gari lililokuwa limebeba wachezaji wa timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys na kulizuia kwa muda.

Kukamatwa kwa gari hilo kulisababisha wachezaji wa timu hiyo inayojiandaa na michuano ya Afcon kwa vijana chini ya miaka hiyo, kushuka ili watafutiwe usafiri mwingine kuelekea walikokuwa wanakwenda.

Msafara wa timu hiyo ulikuwa unakwenda kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye aliwaalika wachezaji na viongozi wa timu hiyo kwa ajili ya chakula ikiwa ni pamoja na kuwaaga rasmi kwa ajili ya safari yao ya kwenda kwenye kambi na baadaye Gabon kwenye michuano hiyo mwezi huu.

Hakikuwa kitendo cha kiuungwana kabisa ambacho kilifanywa na wakala huyo wa TRA na kinapaswa kulaaniwa na kupingwa vikali na wadau wote wapenda michezo hapa nchini, kutokana na ukweli kililenga kuwadhalilisha wachezaji hao na TFF kwa ujumla mbele ya macho ya umma.

Binafsi ninafahamu uhumimu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa letu na sitetei Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutolipa kodi wanayodaiwa, lakini ninapinga na kulaani utaratibu uliotumiwa na wakala huyo hasa kwa kipindi hiki ambacho kila Mtanzania anafahamu timu hiyo ya vijana ipo katika hali gani.

Serengeti Boys kwa sasa ndiyo wamebeba bendera ya taifa, kutuwakilisha katika mashindano makubwa ya soka kwa vijana, kwa hali ya kawaida tu, wakala huyo wa TRA walipaswa kuheshimu hilo kwa mabalozi wetu hao ambao walikuwa tayari wamekabidhiwa bendera ya Taifa na Waziri wa Habari, Uramaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.

Ninaamini kwamba wakala hao wa TRA walikuwa na njia bora zaidi kuliko waliyoifanya ambayo kwanza ilikuwa inadhalilisha timu hiyo, kuwavunjia heshima wachezaji wetu ambao ni mabalozi wetu na pia hata kumvunjia heshima kiongozi wa taifa letu aliyewaalika wachezaji hao.

Madai ya kodi ya TFF na TRA ni ya muda mrefu na kwamba TRA inajua nani hasa wa kumkaba koo kutokana na madai hayo yaliyotokana na malipo ya mishahara ya makocha wa timu ya taifa, Taifa Stars na uratibu wa ujio wa timu ya Taifa ya Brazil mwaka 2010.

Sote tunafahamu kwamba makocha wa Stars walikuwa wakilipwa na Serikali, hasa baada ya Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete, kujitolea kuwalipa makocha hao kutoka Ikulu.

Hivyo basi, TRA wanapaswa kuanza kuihoji Ikulu ambayo ndiyo ilikuwa ikitoa fedha hizo, kisha kuihoji Wizara ya Habari ili kujua ukweli wa kodi hiyo na si kung’ang’ana na TFF pekee ambayo walikuwa waratibu wa kutafuta makocha na pengine waratibu wa mechi dhidi ya Brazil kwa kuwa wao ndio wenye dhamana ya kusimamia soka.

Kwa msingi huo TRA wanatakiwa kuanzia huko juu ili kupata ukweli halisi wa nani alipaswa kulipa kodi hiyo inayodaiwa, maana tangu sakata hilo lianze TFF imekuwa ikisisitiza kwamba mshahara huo ulikuwa ukilipwa na Serikali, lakini TRA wamekuwa wakishikilia msimamo wao.

Ni vyema utafiti ufanyike sasa ili kuweka mazingira wazi na Watanzania wafahamu ukweli wa suala hili maana lilipofikia sasa linaonekana wazi kwamba TRA wanaionea bure TFF. Hivyo, ni wakati mwafaka sasa TRA watoke hadharani na kuuleza umma kwanini wanaikomalia TFF kulipa kodi hiyo hadi sasa wakati ilitakiwa kulipwa na Serikali.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -