Saturday, November 28, 2020

TSHABALALA AANGUKA SAINI SIMBA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA


SIKU moja baada ya BINGWA kuandika beki wa pembeni wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ hajasaini mkataba mpya, uongozi wa vinara hao wa Ligi Kuu Bara umeamua kukata mzizi wa fitina.

Tshabalala au ukipenda Zimbwe Junior ambaye amekuwa na mchango mkubwa kuiwezesha Simba kuongoza ligi hadi mzunguko wa kwanza unakamilika, amesaini Simba mkataba wa miaka miwili jana.

Awali kulikwepo na taarifa ya Tshabalala ambaye alikuwa amebakisha miezi sita katika mkataba wake na Simba kuhusishwa kujiunga na mahasimu wao Yanga kwa dau la Sh milioni 80 kutokana na kile kinachodaiwa Simba kushindwa kukamilisha baadhi ya vipengele kwenye mkataba mpya.

Tshabalala alisaini mkataba huo mbele ya Rais wa Simba, Evance Aveva na meneja wa mchezaji huo, Heri Mzozo.

Akizungumza na BINGWA jana, Mzozo alisema wamemalizana na Simba katika masuala ya msingi japo waligoma kiasi cha fedha alichopewa mchezaji huyo.

“Kuanzia sasa Tshabalala ni  Simba tu, mkataba utakamalizika Julai 30, mwaka 2019, hivyo hakuna matatizo, atakuwa na maisha mazuri ndani ya timu hiyo na mimi sijaona sababu ya kumhangaisha mchezaji huyo, tamaa pia si nzuri, ni vyema ukaheshimu utu,” alisema na kuongeza: “Tukisema thamani hapa tunatafuta kupigwa risasi kwa kuwa kila mtu atataka kujua undani wa fedha hizo, wewe tambua tu amesaini na makubaliano ni siri yetu,” alisema Mzozo.

Awali ilidaiwa Tshabalala alihitaji Sh milioni 60, ikiwa ni ongezeko la Sh milioni 48,000 katika mkataba mpya.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -