Tuesday, October 27, 2020

TSHABALALA AKOGA NOTI

Must Read

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo,...

Katwila: Sitaidharau Mbeya City

NA VICTORIA GODFREY KOCHA wa timu ya Ihefu, Zuberi Katwila, amesema hawaraidharau  Mbeya City...

Kocha apokea kipigo kwa shingo upande

 NA  VICTORIA GODFREY KOCHA wa timu ya Mwadui, Khalid Adam, amesema amesikitishwa na kipigo...

NA MARTIN MAZUGWA

BEKI wa kushoto wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, amekoga noti baada ya mashabiki wa timu hiyo kumchangia fedha kutokana na uwezo wake wa kusakata kabumbu.

Mashabiki wa timu hiyo, walimchangia fedha baada ya kumalizika kwa mazoezi yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Boko Veterani nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Katika mazoezi hayo, mashabiki wa timu hiyo walionekana kuvutiwa zaidi na beki hiyo kutokana na uwezo wake wa kujiamini, kuondoa mashambulizi na kumiliki mipira.

Mashabiki hao walionekana kuchangishana noti ya Sh 5,000 na 10,000 na baadaye kumpa beki wao kutokana na kuridhishwa na uwezo wake wa kujituma uwanjani.

“Navutiwa sana na aina ya uchezaji wa Tshabalala, ni mchezaji mzuri ambaye amekuwa akijitolea ili timu ipate ushindi,” alisema shabiki mmoja.

Simba wanaendelea na mazoezi katika uwanja huo kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo,...

Katwila: Sitaidharau Mbeya City

NA VICTORIA GODFREY KOCHA wa timu ya Ihefu, Zuberi Katwila, amesema hawaraidharau  Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu...

Kocha apokea kipigo kwa shingo upande

 NA  VICTORIA GODFREY KOCHA wa timu ya Mwadui, Khalid Adam, amesema amesikitishwa na kipigo cha mabao 6-1 kutoka kwa...

KMC kumaliza hasira kwa Gwambina

NA WINFRIDA MTOI BAADA ya kuchezea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Yanga, kocha msaidizi wa timu ya Manispaa...

Tshishimbi atambulishwa kuvaa uzi wa AS Vita

NA MWENDISHI WETU KIUNGO wa zamani wa timu ya  Yanga, Papy Tshishimbi, ametambulishwa katika kikosi cha AS Vita ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -