Wednesday, October 28, 2020

Tshabalala mbioni kutua Yanga

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MARTIN MAZUGWA NA ZAINAB IDDY

KAMA Utani tu. Usishangae ukisikia beki wa kushoto wa timu ya Taifa ya Tanzania na vinara wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, anatua Yanga kwenye dirisha dogo la usajili.

Uongozi wa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara  wameamua kuongeza mtu wa kusaidiana na Haji Mwinyi na Oscar Joshua ambaye pia anaelezwa hana muda mrefu wa kuendelea kuwamo kwenye kikosi cha Yanga na chagua lao la kwanza kwa sasa ni Tshabalala.

Kama kawaida yao wazee wa kutibua mambo ya Simba, wakati Wanamsimbazi wakiwa kwenye mazungumzo ya mwisho ya kumpa mkataba mpya Tshabalala baada ya ule wa awali kufika kikomo mwezi huu, Yanga wameelezwa kupenyeza maneno yao kwa beki huyo na kumwahidi dau nono.

Simba wamefanya siri kubwa juu ya kumalizika kwa Tshabalala, lakini siri hiyo imevuja baada ya anayedaiwa kuwa Meneja wa mchezaji huyo kuliweka wazi suala hilo katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.

Taarifa ambazo BINGWA limezinasa kutoka  ndani ya Yanga, zinasema kuwa kuna asilimia 75 mchezaji huyo akavaa uzi wa kijani na njano katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaoanza Desemba 17, mwaka huu.

Taarifa hizo zinasema moja ya vitu vinavyoweza kumuondoa Tshabalala Simba ni uongozi wa Wanamsimbazi kushindwa kumboreshea mkataba wake mpya ambao bado hajausaini huku Yanga.

“Tumeshaanza mazungumzo na mlinzi huyo wa kushoto ambaye yupo kwenye kiwango bora hivi sasa akiwa amecheza michezo yote ya mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

“Tumeangalia beki wa kushoto wa Yanga bado inaonekana Mwinyi ndiye wa kutegemewa, kwani Oscar muda wake unahesabika ndani ya Yanga hivyo lazima atafutwe mbadala wake ambaye atasaidiana na Haji, naye si mwingine ni Tshabalala.

“Taarifa tulizozipata kutoka kwa mtu wa karibu wa Tshabalala zinaeleza kuwa Simba wamefanya mazungumzo na Tshabalala ya kumpa mkataba mpya kipindi kile walipomzawadia gari, lakini wanaweza wakashindwa kuendelea naye kutokana na mchezaji mwenyewe kuomba aboreshewe mkataba wake, jambo ambalo siku zote kwa Simba inakuwa tatizo nasi tutatumia nafasi hiyo kumvuta kwetu,” alisema mtoa habari huyo ambaye hakutaka kuwekwa wazi jina.

Katika hatua nyingine, kiungo mkabaji anayewaniwa na timu hiyo kutoka Zesco ya Zambia, Meshack Chaila, amesema anasubiri  Yanga kukamilishana na alieyekuwa kocha wake, George Lwandamina, ili naye atue nchini wakati wowote.

BINGWA ndio lililokuwa la kwanza kuripoti juu ya ujio wa beki huyo tegemeo wa kikosi cha kwanza cha Zesco na timu ya taifa ya Zambia.

Gazeti hili liliripoti  pia juu ya kuja kwake jijini Dar es Salaam Novemba 15, mwaka huu kwa ajili ya kuingia kandarasi ya miaka miwili na Yanga baada ya kufikia mwafaka wa kuvunja mkataba wake na Zesco.

Akizungumza na BINGWA kwa njia ya Mtandao, Chaila alisema mipango ya kuja Yanga inafanywa na aliyekuwa kocha wake Lwandamina ambaye anaelezwa kwamba yupo nchini.

“Mipango ya kuja huko inafanywa na kocha Lwandamina ambaye ndiye aliyependekeza jina langu kwa uongozi wa Yanga, ninachosubiri ni kuambiwa nije mara baada ya kukamilisha ratiba zangu za timu ya Taifa,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -