Sunday, January 17, 2021

TSHISHIMBI KAMA MATIC

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

Pasi zilizofika 40

Mashuti aliyopiga 2

Kupokonya mpira 3

Rafu alizochezewa 3

NA ALLY KAMWE

SASA mashabiki wa Yanga wanaweza kwenda Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuishuhudia timu yao ikipambana na Simba SC, huku wakitafuna Diamond Karanga. Unajua kwanini?

Kiwango kilichoonyeshwa na kiungo wao mpya, Papy Kabamba Tshishimbi, kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Jamhuri ya visiwani Pemba jana, si cha nchi hii kabisa.

Kwenye pambano hilo lililomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kutokaba na bao lililofungwa kwa mpira wa adhabu na beki wa kushoto, Haji Mwinyi, Tshishimbi alicheza kwa dakika 45 tu na kukonga nyoyo za mashabiki waliofika katika dimba la Gombani, Pemba na wale waliokuwa wakifuatilia mchezo huo kupitia luninga.

Akicheza kwa kujiamini, Tshishimbi aliimudu vyema nafasi ya kiungo, akicheza kwa staili ya kukaba na kushambulia ‘box to box midfielder’, tofauti na wengi walivyotarajia kuwa atakaba tu.

Staili hii ya uchezaji ya Tshishimbi, inafanana na ile anayoitumia kiungo mpya wa vinara wa Ligi Kuu England, Manchester United, Nemanja Matic.

Matic amekuwa akipangwa kiungo wa chini (namba 6), lakini amekuwa akimudu vyema nafasi hiyo pamoja na kupandisha timu na kupiga mashuti makali kwenye lango la wapinzani.

BINGWA lilizifuatilia kwa makini dakika 45 za Tshishimbi alizocheza kwa mara ya kwanza akiwa na jezi ya Yanga na kubaini vitu vikubwa vitatu kutoka kwa kiungo huyo wa zamani wa klabu ya Mbanane Swallows ya nchini Swaziland.

Kwanza, Thishimbi ni mzuri kwa kupiga pasi za chini, fupi na ndefu zinazofika kwa wachezaji wenzake, ambapo katika dakika 45 dhidi ya Jamhuri, alipiga jumla ya pasi 40.

Katika idadi hiyo ya pasi, asilimia 25 alizipiga akiwa ndani ya nusu duara ya eneo la ulinzi na asilimia 15 alizipiga kati ya nusu ya eneo la wapinzani.

Kwa kumtazama Matic kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya West Ham United, Msebria huyo alipiga jumla ya pasi 87, katika dakika 90 alizocheza, hivyo kama Tshishimbi angecheza kwa zaidi ya dakika 45, angekuwa na uwezo mkubwa wa kufikisha idadi hiyo ya pasi.

Pili, Tshishimbi alionyesha umahiri mkubwa wa kukaba na kupokonya mpira kwa wapinzani. Ndani ya dakika 45 alizocheza, alipokonya mpira mara nne hii akifanya kwa mipira ya chini na ile ya juu.

Lakini, Mkocongoman huyo mwenye rasta kichwani kama kiungo mwenzake, Thabani Kamusoko, ni mzuri kwa kupiga mashuti ya nje ya 18 ambapo katika mashuti yake mawili aliyopiga, moja lililenga lango la nyingine kutoka nje kwa sentimita chache.

Kama haitoshi, Tshishimbi ni mkali wa kukokota mpira (dribbling) na hii ilikuwa ikiwapa wakati mgumu viungo wa Jamhuri ambao walijikuta wakimchezea rafu mara tatu ili kumdhibiti.

Kwa namna kocha George Lwandamina alivyokipanga kikosi chake, ni wazi kwenye mchezo dhidi ya watani wao wa jadi, Simba SC, keshokutwa atatumia viungo watatu, akimpanga Tshishimbi kama namba sita, Kamusoko namba nane na kinda Raphael Daudi, akicheza nyuma ya straika kama namba 10.

Safu ya ushambuliaji huenda akaanza na washambuliaji watatu, akitumia mfumo wa 4-3-3, akiwapanga Ibrahim Ajib, Donald Ngoma na Amissi Tambwe.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -