Wednesday, September 30, 2020

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

Must Read

KISA KONA YA CARLINHOS… ...

NA ZAINAB IDDY BAO la Yanga lililofungwa na Lamine Moro juzi katika mchezo dhidi...

HUYU MUGALU ATAWALAZA WATU NA VIATU TU!

NA ONESMO KAPINGA HAKIKA sijapata utamu wa mshambuliaji mpya wa Simba, raia wa DR...

Wachezaji Gwambina wapewa muda

NA ZAINAB IDDY KOCHA wa timu wa  Gwambina, Fulgence Novatus, amesema amewapa muda wachezaji wake ...

NA ZAINAB IDDY

KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard Morrison, aliyesaini mkataba wa miaka miwili Simba kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano mingine.

Tshishimbi kwa sasa ni mchezaji huru, baada ya mkataba wake na klabu ya Yanga kufikia tamati msimu wa ligi uliomalizika hivi karibuni huku wakishindwa kuelewana ofa ya kuongezewa mkataba mpya.

Kiungo huyo alikataa kusaini mkataba mpya, baada ya Yanga kutaka kumpa sh. milioni 60 za usajili huku mwenyewe akihitaji sh. milioni 80 kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Habari zilizopatikana jana kutoka ndani ya klabu ya Simba, zilisema Tshishimbi amekubali kuingia mkataba wa miaka miwili ili kuchukua nafasi ya kiungo Mbrazil Gerson Fraga aliyeomba kuondoka.

“Jana Tshishimbi alikuwa ofisi za Simba kwa zaidi ya masaa matatu akizungumza nao na tayari wamekubaliana baadhi ya mambo, lakini wamempa mkataba wao ili akausome, kisha aurejeshe kwa ajili ya kusaini,”

BINGWA lilimtafuta Tshishimbi ili kujua ukweli wa jambo hilo, alisema kwa sasa ni mchezaji huru  huku akikiri kufanya mazungumzo na timu za Ligi Kuu Tanzanai Bara, licha ya kutozitaja.

“Baada ya Yanga kutangaza kuniacha zipo timu zilikuja na kuzungumza na mimi, sio vizuri kuziweka wazi kwa sasa, mambo yakiwa mazuri mtajua wapi nitafanya kazi katika msimu ujao wa Ligi Kuu hapa Tanzania,” alisema Tshishimbi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

KISA KONA YA CARLINHOS… ...

NA ZAINAB IDDY BAO la Yanga lililofungwa na Lamine Moro juzi katika mchezo dhidi...

HUYU MUGALU ATAWALAZA WATU NA VIATU TU!

NA ONESMO KAPINGA HAKIKA sijapata utamu wa mshambuliaji mpya wa Simba, raia wa DR Congo, Chris Mugalu,kutokana na jinsi...

Wachezaji Gwambina wapewa muda

NA ZAINAB IDDY KOCHA wa timu wa  Gwambina, Fulgence Novatus, amesema amewapa muda wachezaji wake  ili aweze kutathimini kiwango cha...

Kisu amfunika vibaya Manula

NA ZAINAB IDDY KIPA  wa timu ya Azam, David Kisu, amemfunika Aishi Manula  wa Simba kutokana na kutoruhusu...

Zahera awapa Simba taji mapema

NA ZAINAB IDDY BAADA ya Gwambina kufungwa mabao 3-0 na Simba  katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -