Monday, August 10, 2020

Tshishimbi kwisha kazi Yanga

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

NA WINFRIDA MTOI

MJADALA wa kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi wa kuendelea kucheza katika kikosi hicho, umeshafungwa baada ya uongozi kuamua kumpiga chini jumla kutokana na mambo matatu, ikiwamo kudengua kusaini mkataba mpya.

Kumekuwa na mvutano wa muda mrefu juu ya kiungo huyo kusaini mkataba mpya kuitumikia timu hiyo, akidaiwa kuhitaji fedha nyingi.

Mkataba wa Tshishimbi unamalizika rasmi leo, lakini inadaiwa kuwa tangu alipopewa mkataba mpya asaini, amekuwa akizungusha.

Kutokana na jeuri hiyo, uongozi wa Wanajangwani hao umeaona hakuna sababu ya kuendelea kumganda mchezaji huyo wakati kuna wengine wanataka nafasi ya kuchezea Yanga.

Mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema walikuwa wamempa ofa hiyo Tshishimbi kutokana na msaada alioutoa kikosini hapo, japo hakustahili.

Kiongozi huyo alisema moja ya sababu zinazomfanya Tshishimbi kutostahili kupewa mkataba mnono ni kutokana na ukweli kwamba kwa sasa hawezi mikiki mikiki ya kikosi hicho kulingana na malengo waliyojiwekea kwani ana jeraha kubwa litakalomfanya asicheze katika kiwango cha juu.

“Tulipofikia, tumeona tuachane tu na Tshishimbi, atatusumbua; kwanza mkataba huo na kiasi cha fedha tulichotaka kumpa ni kutokana na kuthamini msaada wake kwa Yanga kwa kipindi chote alichokuwa nasi, lakini si kwa kiwango, ukizingatia amekuwa akikabiliwa na majeraha ya mara kwa mara ambayo ni ya muda mrefu hivyo hawezi kucheza katika kiwango cha awali,” alisema.

Alisema kuwa kingine kilichowafanya waamue kuachana na kiungo huyo, raia wa DR Congo, ni kitendo chake cha kuwadengulia viongozi wa Yanga, akionesha jeuri wazi wazi.

“Lakini pia tusisahau Papy anadaiwa kuchangia katika kipigo tulichopewa na Simba (walipofungwa mabao 4-1). Naye anatajwa katika orodha ya wachezaji waliotuua na ndio maana alilazimisha kucheza akijua ni majeruhi kwa kuwa ile ilikuwa ni mipango maalum,” alisema.

Hivi karibuni, Kaimu Katibu Mkuu Patrick Simon, alisema walimpa Tshishimbi siku 14, kuhakikisha anasaini mkataba huo na akishindwa, rasmi wanaachana naye.

Kauli hiyo inaonekana kujibiwa kwa vitendo, kwani Wanajangwani hao wameamua kufanya kweli kwa kushusha mbadala wa Tshishimbi ambaye ni kiungo fundi kutoka Kagera Sugar, Zawadi Mauya.

Mauya alisaini mkataba wa miaka miwili Yanga jana, mbele ya Simon na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Hersi Said. 

Sifa mojawapo ya Mauya ni kiungo anayejua kukaba na kupiga pasi zenye macho.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alithibitisha usajili huo na kusema huo ni mwanzo katika mkakati wao wa kuimarisha timu yao tayari kuuwasha moto msimu ujao.

“Kama tulivyowaambia mashabiki wa Yanga kuwa tutaboresha kikosi chetu ili msimu ujao tufanye vizuri, tumeanza na wachezaji wa ndani na tutaendelea hadi wale wa kimataifa tunaowataka,” alisema Mwakalebela.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -