Tuesday, November 24, 2020

TUITUMIE NGUVU YA SANAA KATIKA KUITANGAZA NCHI YETU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NI mwezi mpya, ni matumaini yangu kwamba tuko pamoja katika safu hii. Nawashukuru wadau ambao ni wasomaji wangu. Nimekuwa nikisisitiza mara nyingi hapa kuwa kwa nchi zilizoendelea mapato yao makubwa yanatokana na mambo matatu, teknolojia, sanaa na michezo.

Mambo matatu tu, nikisema teknolojia, ninamaanisha mambo yote yanayohusisha madini, utalii na mambo mengine nje ya hayo nchi kubwa hizi wanawekeza sana kwenye michezo na sanaa, kwa sababu chakula kwa nchi kubwa si jambo linalowasumbua tena.

Jaribu kuangalia watu tunaowatambua sisi watu wa dunia ya tatu, mara nyingi ni wasanii na wanamichezo wao. Ukiangalia kwa makini utaelewa kwamba wenzetu walijua hili mapema tu kwamba nguvu inayopatikana kwenye sanaa hasa za maonyesho ni kubwa sana, labda tuseme hivi tukiacha Rais wa Marekani, Donald Trump, tunamjua waziri wake yeyote? Labda kama uwe mtu unayefuatilia sana mambo ya siasa za Marekani.

Jambo la kushangaza nikiuliza swali kuhusu wasanii wa Marekani hapa nitatajiwa majina mpaka ya mababu zao na wanakoishi au nitatajiwa mpaka chipukizi wa kwenye American Idol, kwanini? Kwa sababu sauti zao ni kubwa sana na zinavuma sana.

Marehemu Mzee Mwinamira aliimba hapa nyimbo ya madereva kulewa miaka ile 1970,80, ndio leo tunagundua mpaka tochi za askari wa barabarani, vidhibiti mwendo, stika za barabarani, simu za taarifa za ajali na mambo mengine kama hayo.

Lakini Mzee Mwinamira aliliona hili miaka ile, hebu fikiri, marehemu Dk. Remmy Ongalla, aliimba mambo kwa soksi miaka ile ya 1980-90 ukafungiwa ule wimbo, baadaye tukaanza kugawa kondom kama njugu, fasiri ya Remmy ilizimwa kufikisha ujumbe ambao pengine wakati tunazinduka kugawa kondom kusingehitajika nguvu kubwa ya uelimishaji kama wimbo wa Mambo kwa Soksi wa Dk. Remmy ungeachwa.

Tusichokijua ni kwamba nguvu ya sanaa ni kubwa mno kiasi kwamba, zipo nyimbo ambazo zimetumika kwenye mitihani ya kidato cha nne kama mwimbo wa Marijani Rajabu wa Mwanameka. Na ziko nyimbo nyingi ambazo zimetumika kwenye mambo mazito katika dunia hii, ndio maana nasistiza tunachelewa sana kutumia sanaa kama chombo madhubuti ambacho pia kingeweza kutupa utambulisho kama taifa.

Wapo watoto wa kawaida tu hapa nchini wanausikia tu Mlima Kilimanjaro, tena inawezekana hawajui ulipo, lakini nenda Rufiji kule kaulize mtu yeyote kijana kuhusu Diamond atakwambia mpaka alipoanzia maisha pale Tandale. Yaani ukitaja tu jina la Diamond bila kujali kwamba unamaanisha madini ya almasi yanayopatikana Mwadui, Shinyanga, mtu anamhusisha mwanamuziki hii ni kwa sababu ya nguvu ya sanaa.

Zunguka sehemu mbalimbali muulize mtu kuhusu Katiba katika kipengele kimoja tu wengi hawajui, lakini muulize kuhusu Wema Sepetu au msanii yeyote atakupa habari zake, kwanini, sanaa ni kioo kinachokuonesha hali halisi ilivyo kwenye kijiji, kata, kitongoji, mtaa, wilaya, mkoa, hatimaye mji.

Sanaa kwa miaka mingi sana tangu tulipopata Uhuru ilifanya kazi kubwa sana, nakumbuka msanii mahiri wa Afrika Kusini, Dorothy Masuka, alisema alifanya kazi ya kuzunguka mikoa mbalimbali ya Tanzania wakati huo kutoa elimu kwa kutumia sanaa.

Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliamini kwenye nguvu ya sanaa katika kufikisha ujumbe, wasanii walifanya kazi kubwa kueneza falsafa ya Ujamaa na kujitegemea na pia katika kampeni mbalimbali za kitaifa ambapo wasanii walitumika katika kutunga nyimbo.

Marekani taifa kubwa kabisa duniani, liliamini katika sanaa, wakati wanataka kuingia kwenye vita ya pili ya dunia, kitengo maalumu cha vita, kiliamua kutumia wasanii kuandaa filamu zilizoonyesha uwezo wa kivita wa Marekani ili kuwashawishi wananchi kukubali nchi yao kuingia katika vita ya pili.

Ni kwa kutumia sanaa walifanikisha kuwashawishi wananchi na hasi sasa Marekani wanatumia propaganda za filamu za kivita kuitisha dunia, kuonyesha kwamba ni taifa lenye makomandoo wa kutisha na mitambo ya nguvu zaidi.

Kwa sisi ni wazi kwamba jamii, Serikali, wasanii, tuwekeze nguvu ya pamoja kujenga misingi mizuri na imara kwenye sanaa zote, baada ya miaka mitano tu tutaona namna ambavyo tunaibadilisha Tanzania kuwa marufu na yenye kutambulika kimataifa, mfano mzuri ni msanii Diamond, amebeba jina Tanzania mgongoni kwa sasa, wapo wengi waliofanya hivyo miaka ya nyuma, lakini hatukuwatumia ipasavyo kujitangaza. Kwa sasa lazima tuamke utalii wetu utatangazwa vyema zaidi na wasanii kama tutaamua kuwatumia.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -