Wednesday, November 25, 2020

TUKIAMUA TUNAWEZA KUTENGENEZA AKINA SAMATTA LUKUKI KUPITIA VPL

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAINAB IDDY

LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kwa sasa inaelekea ukingoni ambapo zimebaki mechi sita tu kukamilisha msimu huu, huku timu za Simba na Yanga zikionekana kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kutwaa ubingwa, japo hata Azam wanaweza kuibuka kidedea iwapo watakaza ‘msuli’ vilivyo, lakini ikiombea vigogo hao wa soka nchini waboronge.

Tofauti na misimu iliyopita, ligi ya safari hii inatarajiwa kumalizika ikiwa katika sura mpya kabisa ambayo hasa imeletwa na Mtanzania, Mbwana Samatta, anayekipiga katika timu ya Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji.

Hivi karibuni, Samatta alifanya mambo makubwa akiwa na timu ya Taifa, Taifa Stars, katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotambulika na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) dhidi ya Botswana uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Samatta alionyesha kiwango cha hali ya juu, akifunga mabao mawili safi yaliyoiwezesha Stars kushinda mabao 2-0, kiasi cha kuwakosha vilivyo mashabiki waliofika uwanjani na wale waliokuwa wakiufuatilia mchezo huo kupitia runinga.

Kwa kiasi fulani, cheche za Samatta zimeonekana kuanza kurejesha msisimko wa soka hapa nchini kwani ilionekana wazi mashabiki kupoteza matumaini na timu yao ya Taifa, hasa baada ya Tanzania kuporomoka kwa kasi kubwa katika viwango vya ubora vya Fifa.

Na sasa stori kwenye vijiwe mbalimbali, vyombo vya usafiri na hata makazini kama si majumbani, ni itakuwaje iwapo Tanzania itafanikiwa kuzalisha wachezaji zaidi watakaopata nafasi za kuonyesha cheche zao kwenye ligi za Ulaya?

Kwa kuwa moja ya siri ya kupata wachezaji bora ni kuwa na ligi bora, imeonekana wazi kwamba Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), ndiyo mkombozi wa soka letu, lakini tu iwapo itapata usimamizi stahiki chini ya watendaji watakaohakikisha wanafuata sheria zote 17 za mchezo huo, huku wadhamini nao wakitimiza wajibu wao kwa wakati.

Juu ya usimamizi wa ligi na nafasi ya Tanzania kuzalisha akina Samatta wengi zaidi, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Luicas, anasema: “Hakuna ubishi kuwa ligi yetu bado ni bora pamoja na changamoto kadhaa zinazotukabili. Iwapo kila mmoja atatimiza majukumu yake bila ujanja ujanja tunaweza kufika mbali.”

Anasema kama jinsi Samatta alivyoweza kupasua anga hadi Ulaya, ndiyo hivyo hata wachezaji wengine wanaoshiriki Ligi Kuu Bara wanaweza kufika mbali iwapo watazingatia miiko ya soka, wakijituma kadiri ya uwezo wao, kuzingatia nidhamu na zaidi kuwa na malengo ya kufika mbali badala ya kuridhika na mafanikio kiduchu wanayoyapata.

Kwa upande wake, winga wa Yanga, Simon Msuva, anasema binafsi amekuwa akiumiza kichwa ni vipi anaweza kufika mbali katika mchezo huo, ikiwezekana kufikia au hata kuyapita mafanikio ya Samatta ambaye kwa sasa ndiye balozi wa Tanzania katika ulimwengu wa soka.

“Hakuna kisichowezekana chini ya jua, kikubwa ni wachezaji kujituma, kuzingatia nidhamu na kubwa zaidi kujiwekea malengo ya kufika mahali fulani. Naamini ligi yetu bado ina uwezo wa kutoa nyota watakaofanya mambo makubwa huko Ulaya kama anavyofanya Samatta,” anasema Msuva ambaye kwa sasa ndiye kinara wa mabao VPL, akiwa ameshacheka na nyavu mara 12.

Anaongeza: “Wapo wachezaji wengi wanakwenda kufanya majaribio nje na wanafaulu, lakini hawaendi, hivyo ili kuwe na akina Samatta wengi, ni lazima mfumo ubadilike kuanzia TFF, klabu na hata sisi wachezaji tujue kipi tunataka kwenye maisha yetu ya mpira.”

Naye kiungo wa Simba, Jonas Mkude, anasema: “Binafsi sina shaka na ligi yetu, tatizo ni wasimamizi ambao wakati mwingine wamekuwa wakiwakwamisha wachezaji wanapotaka kupiga hatua mbele. Umefika wakati viongozi waangalie mbele, kila Mtanzania anatamani kuona nchi yetu ikiwa na wachezaji wengi zaidi wanaocheza Ulaya kitu ambacho kinawezekana kabisa.”

Kigi Makasy wa Ndanda, anasema Tanzania ina wachezaji kibao wenye uwezo wa kufanya mambo makubwa Ulaya kama anavyofanya Samatta, ila tatizo ni ubabaishaji wa baadhi ya viongozi. “Tukiacha ubabaishaji, ligi yetu inaweza kuwa maarufu duniani kwa kutoa wachezaji watakaokuwa tishio katika ligi mbalimbali hasa Ulaya,” anasema winga huyo aliyewahi kukipiga Yanga na Simba kwa mafanikio makubwa.

Naye mshambuliaji wa Azam FC, Khamis Mcha, anasema ili kuwe na akina Samatta wengi ni lazima msingi imara uanzie TFF, timu pamoja na wachezaji wenyewe.

“Mafanikio ya Samatta ni juhudi zake binafsi alizozionyesha kwa kipindi hicho jambo ambalo hivi sasa ni gumu, kwani mara nyingi tumeona wachezaji wanapata nafasi ya kucheza soka la kulipwa, lakini hawaendi, ukijaribu kuchunguza sababu, utagundua mfumo mbovu uliopo kwenye timu wanazozitumikia.

Naye winga wa Simba, Shiza Kichuya, anasema: “Ili wachezaji tufike mahali alipo Samatta, ni lazima kwanza sisi wenyewe tujitambue, tujitume, tujilinde, lakini pia ligi iwe bora pamoja na mifumo huru katika timu tunazozitumikia.

“Iwapo kama wachezaji tutakuwa na ndoto za kuwa kama Samatta halafu hatuna njia, mwongozo wala sapoti ya kutuunga mkono katika hili, tutaishia kila siku kusema tunayatamani mafanikio ya mwenzetu pekee, kitu ambacho si kizuri hasa kwa sisi wachezaji wadogo tunaoanza kusaka mafanikio,” anasema.

Akizungumzia juu ya udhamini wao, Meneja Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu, anasema: Ni fahari kubwa kwetu kudhamini ligi hii yenye msisimko wa aina yake na hivyo kutoa fursa kwa wapenzi wa soka nchini na kwingineko kupata burudani ya aina yake kupitia kabumbu.”

Anasema wanafarijika kujiona sehemu muhimu ya mafanikio ya timu katika ligi hiyo, lakini pia mafanikio ya Samatta huko Ulaya kwani naye alitokea VPL ambapo baada ya kufanya vema, alionwa na TP Mazembe ya DRC iliyomchukua na kuibeba mno katika Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Mtanzania huyo akitwaa tuzo ya mfungaji bora.

“Iwapo kila mmoja atatimiza majukumu yake ipasavyo, tunaweza kuwapata akina Samatta hata zaidi ya 10 hali itakayoifanya Tanzania kuwa tishio kimataifa. Tunawaomba wadau wote wa soka kuungana na Vodacom katika kuisapoti ligi hii kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuendeleza michezo na hivyo kupunguza tatizo la ajira linalowakabili vijana wengi, lakini pia kuwaepusha na utumiaji wa dawa za kulevya kwani wakiwa wanashiriki michezo, hawawezi kupata muda wa kufanya matendo maovu, yakiwamo ya ukabaji na mengineyo kama hayo,” anasema Nkurlu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -