Monday, November 30, 2020

TUKIPATIA HAPA, TUTARAJIE AKINA SAMATTA KIBAO ULAYA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwaka 2019.

Wakati Watanzania wakijiandaa kushuhudia michuano hiyo ikifanyika hapa nchini, Tanzania imefanikiwa kufuzu fainali za mwaka huu zinazotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu nchini Gabon.

Tayari timu yetu ya Taifa ya vijana wenye umri huo, Serengeti Boys, imeanza maandalizi kabambe kuhakikisha inafanya vema kwenye fainali za mwaka huu.

BINGWA tunaamini kuwa iwapo timu yetu hiyo itafanya vema, japo kufika hatua ya nusu fainali au hata fainali, hali hiyo inaweza kuongeza hamasa ya wapenzi wa soka na Watanzania kwa ujumla katika suala zima la maandalizi ya fainali za mwaka 2019.

Kama kila mmoja wetu anavyofahamu, uenyeji wa fainali kama hizo si jambo la mchezo mchezo kiasi kwamba kunahitajika kufanyika maandalizi ya kina, kuanzia kwa timu hadi suala zima la uhamasishaji kuhakikisha kila mmoja anajitolea kadiri ya uwezo wake kufanikisha tukio hilo adimu.

Sambamba na hilo, BINGWA tunaamini ushiriki wa fainali za mwaka huu na uenyeji wa zile za 2019, unaweza kuwa na faida nyingine kwa soka la Tanzania kwa kuona ni vipi hilo linaweza kuwa chachu ya kuvumbua vipaji zaidi vya soka hapa nchini.

Katika hilo, tunaamini hiki ni kipindi muhimu mno kwa kuhakikisha vijana wenye vipaji wanapewa fursa ya kucheza mpira na hatimaye waweze kutoa mchango wao kwa timu ya taifa na hatimaye kufanya vema 2019 na hivyo kujitengenezea soko kwenye klabu mbalimbali za Ulaya.

Hivi karibuni, Kampuni ya New Habari (2006) wazalishaji wa magazeti ya Bingwa, Dimba, Mtanzania, Rai na The African, ilifanikiwa kudhamini mchakato wa kusaka vipaji kwa wanafunzi waliomaliza darasa la saba mwaka jana waliokuwa na vipaji vya hali ya juu, walipata udhamini wa masomo katika shule ya Lord Baden Memorial iliyopo Bagamoyo, mkoani Pwani ambayo pamoja na kufundisha masomo ya kawaida, inaendeleza vipaji katika fani mbalimbali.

Katika mpango huo ulioendeshwa kwa ushirikiano na shule hiyo chini ya Mkurugenzi wake, Kanali mstaafu Iddi Kipingu, vijana kutoka mikoa mbalimbali walionyesha vipaji vya hali ya juu na kuthibitisha kuwa iwapo kutafanyika michakato kama hiyo kwa wingi kabla ya 2019, Tanzania inaweza kuwa na vijana lukuki watakaoiwezesha kufanya vema kwenye fainali za mwaka huo.

Hivyo basi, pamoja na wale vijana wanaolelewa na TFF, kunatakiwa kuwapo kwa vituo vingine vingi vya kulea na kuwaendeleza vijana wenye vipaji vya soka ili angalau uenyeji wetu wa fainali za 2019 uwe wa ufanisi na hivyo kutoa vipaji vitakavyofuata nyayo za kaka yao, Mbwana Samatta anayetesa huko Ulaya akiwa na kikosi cha Genk ya Ubelgiji.

Chonde chonde Watanzania, kila mmoja ajitoe kadiri ya uwezo na nafasi yake kusaidia maandalizi ya ushiriki wa Serengeti Boys katika fainali za Afrika za mwaka huu na zile za 2019 ambazo tutakuwa wenyeji.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -