Monday, October 26, 2020

TUKIWEKEZA KATIKA NDONDI TUTATOKA

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

PAMOJA na ukweli kuwa soka ndio mchezo unaopendwa zaidi duniani, kwa hapa nchini umeshindwa kuwatendea haki Watanzania kutokana na timu zetu kuanzia zile za klabu hadi za Taifa, kuboronga katika mashindano ya kimataifa.

Tangu timu yetu ya Taifa, Taifa Stars ilipofuzu fainali za Afrika mwaka 1980, haijawahi kufika mbali kwenye anga ya kimataifa zaidi ya kuishia hatua za awali.

Hali imekuwa hivyo miaka nenda rudi pamoja na soka kupewa kipaumbele na Serikali takribani zote nne zilizopita tofauti na ilivyo kwa michezo mingine.

Ni kutokana na hali hiyo, Watanzania wapenda michezo wamekuwa wakisononeka na kufikia kukata tamaa ya kushabikia timu zao, kuanzia zile za klabu hadi za Taifa na kuamua kuhamishia mapenzi yao kwa timu za Ulaya.

Na kwa sasa hali inaonekana kuwa mbaya zaidi kwani Tanzania imezidi kuporomoka kwenye viwango vya soka vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), ikishika nafasi ya 156 ikiwa ni nafasi ya chini mno kuwahi kutokea.

BINGWA tukiwa kama wadau wa soka, tumekuwa tukiguswa na kuendelea kudorora kwa soka letu pamoja na mchezo huo kupewa sapoti ya hali ya juu kutoka kwa mtu mmoja mmoja, taasisi, mashirika, kampuni na hata Serikali.

Lakini pia, kwa kuwa tu-wadau wa michezo mingine, tunadhani kuna umuhimu wa Watanzania kuhamishia hisia zetu katika michezo mingine kama ndondi, riadha, mpira wa kikapu, netiboli, wavu, kuogelea na hata mieleka.

Tunadhani iwapo michezo hiyo hasa ndondi na riadha itapewa sapoti kama ilivyo katika soka, inaweza kutuletea heshima kubwa kama ilivyokuwa zamani enzi za wanariadha Filbert Bayi na wenzake pamoja na mabondia Emmanuel Mlundwa, Michael Yombayomba, Habibu Kinyogoli ‘Masta’, Stanley Mabesi ‘Ninja’, Rashid Matumla ‘Snake Boy’ na wengineo.

Kwa bahati nzuri, angalau riadha wana sehemu ya kujinoa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambako iwapo watapewa sapoti, wanaweza kujipanga upya na kuitangaza vema Tanzania katika anga la kimataifa.

Lakini kwa ndondi ni ‘shida’, hakuna ukumbi wowote rasmi wa kisasa unaoweza kutumika kuwaandaa vilivyo vijana chipukizi wenye ndoto za kufuata nyayo za akina Mlundwa.

Wenye mapenzi na mchezo huo wamekuwa wakijifunza katika mazingira na vifaa duni, huku wakikosa msaada wa kitaalamu.

Ni kutokana na hali hiyo, tunadhani kuna umuhimu wa kuanza kwa kujenga ukumbi wa kisasa wa ndondi ili kutoa fursa kwa vijana wenye vipaji kujiendeleza, lakini pia wakipatiwa msaada wa wataalamu na vifaa vya kisasa pia.

Tumalizie kwa kuwasisitiza Watanzania kuanzia Serikali, mashirika, kampuni na wadau mmoja mmoja kuona umuhimu wa kuisaidia michezo mingine nje ya soka, zaidi ikiwa ni ndondi ambao angalau ulishaitangaza nchi yetu kimataifa miaka iliyopita kama ilivyokuwa kwa riadha.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -