Tuesday, November 24, 2020

TULIONDOA KOCHA BORA STARS, TUMEONDOA TENA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MAREGES NYAMAKA

HATIMAYE hivi karibuni Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi, alitumia akaunti yake ya mtandao wa Twitter kutangaza mabadiliko ya benchi la ufundi la timu ya Taifa, Taifa Stars.

Kocha Charles Boniface Mkwasa ameondoka Stars na sasa nafasi yake inakaimiwa na Salum Mayanga aliyekuwa akiinoa Mtibwa Sugar.

Msingi wa hoja yangu si kupinga kitendo cha TFF kuachana na Mkwasa, ila je, kibarua hicho kimekabidhiwa kwa mtu sahihi na ni kweli Mkwasa alistahili kuchomolewa kwenye wadhifa wake huo?

Ni vigezo gani vilivyotumika kumwona Mayanga kama mtu sahihi wa kupewa kazi ya kuinoa Taifa Stars kuliko Mkwasa mwenye leseni daraja A inayotambuliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF)?

Mbali na hilo, ikumbukwe kuwa baada ya Malinzi kuingia madarakani kilichofuata ni kufukuzwa kwa kocha  Kim Poulsen aliyekuwa akiinoa Stars kwa kipindi hicho na wasaidizi wake wote.

Naamini Kim alikuwa kocha bora kutokana na juhudi zake za kuandaa kizazi kipya cha wachezaji kilianza kuonekana kwa muda mfupi aliokuwa kocha mkuu wa Stars, lakini tulimwondoa na tumemwondoa tena Mkwasa.

TFF waliamini kuwa Martinus “Mart” Nooij ndiye aliyekuwa akifaa kuliongoza benchi la ufundi la timu yetu hiyo na itakumbukwa kuwa kocha msaidizi wa Mholanzi huyo alikuwa Mayanga.

Takwimu zinaonyesha kuwa kwa kipindi chote Nooij na Mayanga walichokuwa Stars, hakukuwa na afadhali ya soka letu.

Katika michuano ya mashindano ya nchi  za Maziwa Makuu (Cosafa), Stars ilitupwa nje kwa aibu kwani iliishia hatua ya makundi huku ikiwa haijashinda hata mchezo mmoja.

Lakini pia, safari ya Stars kuifukuzia tiketi ya kushiriki fainali za Mataifa Afrika za mwaka huu (Afcon 2017) ziliziishia njiani chini ya Nooij akiwa na msaidizi wake Mayanga.

Ukiliweka kando hilo la Afcon 2017, Stars pia iliambulia patupu kwenye michuano ya Ligi ya Wachezaji wa Ndani (Chan), ikiwamo kukumbana na kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Uganda.

Unajua nini kilifuata? Nooij akafungasha kila kilicho chake huku akilipwa kiasi cha fedha kisichopungua Sh milioni100  kutokana na kitendo cha TFF kuvunja mkataba wake wa miaka miwili.

Mpaka anaondoka nchini, Nooij alikuwa ameiongoza Stars katika michezo 18, akashinda mara tatu, akapoteza mechi tisa na kuambulia sare sita.

Kwa hali ya kawaida tu, Rais wangu Malinzi unamrejesha Mayanga Stars kwa mantiki ipi hasa? Ni kitu gani kakifanya kwa muda mfupi uliopita tangu umtimue akiwa chini ya Nooij?

Naheshimu sana uwezo wa Mayanga kwa soka la Tanzania, kutokana na wasifu wake wa kuzinioa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwamo Tanzania Prisons na  Mtibwa Sugar kwa nyakati tofauti.

Lakini bado Mkwasa alistahili kuongoza jahazi hilo la Stars kutokana na muda mfupi aliokaa. Au kuporomoka kwa Tanzania kwenye viwango vya  Shirikisho la Soka Duniani  (FIFA) ndicho kigezo kilichotumika kumng’oa Mkwasa? Haiwezekani.

Licha ya leseni ya daraja A aliyonayo Mkwassa, angewezaje kutimiza ndoto alizokuwa nazo kwa mzingira aliyokuwa nayo?

Nafasi hiyo ikaenda kwa kocha mwenye leseni A ya Caf, Charles Boniface Mkwasa, ambaye alikuwa na mlima mrefu wa kupanda akakaribishwa na sare ya bao 1-1 dhidi ya Uganda, ukiwa ni  mchezo wa marudiano michuano ya Chan.

Bada ya Malinzi kugundua uamuzi wake wa kumtimua Kim Poulsen kuwa ‘alibugi’, baadaye alimrejesha na kumpa nafasi ya mshauri kwa timu za Taifa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -